BUNGENI LEO DODOMA
Msemaji wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Cecilia Paresso, akisoma hotuba mbadala ya wizara hiyo kwa mwaka 2017 na 2018 bungeni mjini Dodoma
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Tizeba akisoma hotuba ya wizara hiyo ya makadirio ya mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2017 na 2018, Bungeni Dododma
SERIKALI imetakiwa kuongeza
nguvu ili kukabiliana na uvuvi haramu nchini kwa kuwatumia askari wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kauli hiyo imetolewa bungeni
jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dk
Mary Nagu, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa
bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/17 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya
wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.
“Pamoja na wizara kupitia
idara ya maendeleo ya uvuvi kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti
vitendo vya uvuvi haramu ambavyo bado vinaendelea kushamiri mahali pengi nchini,
bado vitendo hivyo vinaendelea kutokea.
“Kwa hiyo, kamati inashauri
Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na uvuvi haramu ikiwa
ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya doria
kwenye maeneo ya maziwa ikiwa ni pamoja na kushirikisha Jeshi la Wananchi
katika kufanya doria ili kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu,” alisema Dk. Nagu.
Katika hatua nyingine, alisema
kuna haja Serikali kuwa na kanda maalum ya kilimo cha umwagiliaji ili kND hiyo
iweze kusaidia katika kuinua kilimo nchini.
Naye mseaji wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni katika wizara hiyo, Secilia Pareso, alisema kuna haja Serikali
kuangalia sheria zake ili nyavu zinazotumika kuvulia samaki katika Ziwa
Tanganyika, zitofautiane na zinazotumika katika Ziwa Viktoria kwa kuwa baadhi
ya samaki wanatofautiana ukubwa hasa hasa dagaa.
Pamoja na hayo, alitaka kujua
Serikali itachukua hatua gani za kuwafidia wafugaji ambao mifugo yao ilikufa
kutokana na ukame katika mwaka 2016/17.
Mwisho.
Comments
Post a Comment