MATUKIO MBALIMBALI
Mwenyekiti wa Baraza la Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam Baraza Kuu Sheikh Suleiman Kilemile, akitoa tamko la Masheikh kwa niaba ya Waislamu wa Tanzania Kuhusu mauaji yaliyofanyika Mwanza Katika Masjid ya Rahmaan,Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob, akimsalimia mtoto baada ya kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala, wakati wa Ziara ya Kamati ya Fedha, jijini Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob, akitoka kukagua moja ya jengo la Wodi ya Bima ya Afya katika Hospitali ya Mwananyamala, wakati wa Ziara ya Kamati ya Fedha,(kulia) Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, , Dk Nkungu Daniel Nkungu, Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob,akikagua barabara ya Akachube, wakati wa Ziara ya Kamati ya Fedha, jijini Dar es Salaam
Meya akiruka madimbwi ya maji katika barabara hiyo
MICHEZO YA MKUU WA MAJESHI UWANJA WA UHURU DAR
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Mwakilishi wa MnadhimuMkuu wa Majeshi Meja Jenerali Simoni Mumwi mara baada ya kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Kikosi cha Ngome kikipita mbele ya mgeni wa heshima Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, kutoa heshima wakati wa ufunguzi wa mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa amesimama wakati vikosi vya michezo vikipita kwa gwaride la heshima wakati wa ufunguzi wa mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassor akihutubia wanamichezo wa kijeshi kwenye sherehe za ufunguzi wa mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi Meja jenerali Simoni Mumwi akihutubia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na marefarii pamoja na makamisaa wa michezo wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwatakia heri timu ya Tembo kutoka Ruvuma na Kombaini ya Vikosi vya JKT kabla ya kuanza mechi yao kwenye mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tembo pamoja na Kombaini ya JKT mara baada ya kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
KABWE AAGWA DAR NA MAMIA
Baadhi ya Mawakili na Wanasheria wakiingiza mwili wa
aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bwa. Mbonea Wilson Kabwe katika
viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Familia ya aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe wakifuatilia ibada ya kutoa heshima za mwisho ya kuuaga mwili huo.
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene akiwakisha salamu za rambirambi kutoka Serikalini wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa Paul Makonda akiwasilisha
salamu za rambirambi kutoka ofisi ya Mkuu mkoa wa Dar es salaam wakati wa kutoa
heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam
Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es salaam
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akitoa heshima
za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea
Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Mamba,
Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita akitoa
heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw.
Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea
Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Baadhi ya Ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria ibada ya heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Comments
Post a Comment