MKUU WA WILAYA YA SAME AWATAKA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA MMOMONYOKO WA MAADILI.
NA Ashrack Miraji-----SAME Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amewataka wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo kujiepusha na vitendo vinavyoashiria mmomonyoko wa maadili ikiwemo ushoga, usagaji, mapenzi kabla ya umri pamoja na utoro, akisisitiza kuwa mienendo hiyo inaweza kuhatarisha mustakabali wao na kupelekea kukatisha ndoto zao za kielimu. Akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule akiwa kwenye ziara ya kufuatilia hali ya mahudhurio ya wanafunzi kwa mwaka 2025, Mhe. Kasilda alisema vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinakwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha elimu nchini. “Mimi, kama Mkuu wa Wilaya, nataka ninyi mtimize ndoto zenu. Ni marufuku kujihusisha na vitendo vyovyote vya mmomonyoko wa maadili vikiwemo kujihusisha na mapenzi, usagaji, ushoga pia utoro kwa kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuinua sekta ya elimu,” alisisitiza Mhe. Kasilda. Aidha, aliwasihi wanafun...