Posts

MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MAJI KISARAWE MJINI

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Afisa Mtendaji  Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian  Luhemeja kuhusu Mradi wa Maji wa Kisarawe mjini  akiwa katika siku ya tatu ya ziara ya Mkoa wa Pwani, Novemba 29, 2022. Kushoto  ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua tangi la Maji wakati alipotembelea Mradi wa Maji wa Kisarawe Mjini akiwa katika siku ya tatu ya ziara ya Mkoa wa Pwani, Novemba 29, 2022 .  Kushoto  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange na wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteremka kutoka katika tangi la Maji wakati aliptembelea Mradi wa Maji wa Kisarawe Mjini akiwa   k...

UBUNGO NA LISHE YA WATOTO

Image
Mradi wa kukuza lishe (SUN), wawanufaisha wanawake na watoto  Na PATRICIA KIMELEMETA MANISPAA ya Ubungo imetoa elimu ya lishe kwenye vituo 76 vya kulea Watoto (day care) vilivyopo kwenye Manispaa hiyo ili kuhakikisha kuwa watoto wanaosoma katika shule hizo wanapata lishe bora kwa ajili ya ukuaji wao. Hatua hiyo imekuja kutokana na utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto(PJT-MMMAM) iliyozinduliwa Desemba 2021, itatekelezwa hadi Mwaka 2026, ambayo inahusu watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane. Katika Programu hiyo, Halmashauri zimetakiwa kushirikiana na Asasi za kiraia ili kutekeleza mpango huo na kuwafikia wananchi wengi zaidi Ili waweze kubadili mfumo wa maisha na kulea watoto wao kwa kuzingatia afua tano za Malezi na makuzi. Afua hizo ni pamoja na lishe, afya, elimu, Malezi yenye mwitikio na ulinzi na Usalama kwa watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane. Akizungumza hivi karibuni, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Bupe M...

RAIS SAMIA AWAHIMIZA WATUNZA KUMBUKUMBU KUZINGATIA USIRI

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) kabla ya kufungua Mkutano wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 27 Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo kwa Wadau mbalimbali waliowezesha kufanikisha Mkutano wa 10 wa Chama cha Menejimenti na Kumbukumbuku na Nyaraka Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano...

LISHE

Image
  Wajumbe wa kamati ya utrkelezaji ya Programs Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto(PJT-MMMAM) wakiwa kwenye kikao cha kujadili utrkelezaji wa programu Hiyo mkoa wa Dar Es Salaam.Na Mpigapicha Wetu Na PATRICIA KIMELEMETA HALMASHAURI ya Jiji la Dar Es Salaam, k wa kushirikiana na wadau mbalimbali wa lishe, wameanza kutoa elimu ya lishe kwa watoto wenye umri kuanzia sifuri hadi miaka minane ili waweze kuwa na afya bora na kukuza ubongo wao, jambo ambalo litapunguza udumavu. Uamuzi huo imekuja baada ya Halmashauri hiyo kutekeleza Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ambayo inaanzia umri sifuri hadi miaka minane ambapo kila Halmashauri wanapaswa kushirikiana na Asasi za kiraia kutekeleza afua tano zilizopo kwenye Programu hiyo ambazo ni pamoja na lishe bora, elimu, afya, Malezi yenye mwitikio na ulinzi na Usalama. Ofisa Maendeleo wa Wilaya ya Ilala, Daudi Mpuli amesema kuwa, uamuzi wa kutoa elimu ya lishe kwenye shule hizo ni pamoja...

SERIKALI INATAMBUA MICHANGO YA TAASISI ZA DINI KWA TAIFA-DKT MABULA

Image
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akiwasili katika Kanisa la AICT Kizota tayari kuzindua Dayosisi mpya ya Kanda ya Kati ya Kanisa hilo pia kushiriki kusimikwa na kuwekwa wakfu Askofu Mteule Amos Katoto Ngeze kuwa Askofu wa kwanza wa kanisa la African Inland Church Dayosisi ya kati Dodoma. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akiweka tayari kukata utepe kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kanisa Kuu la Africa Inland Church Tanzania Dayosisi ya kati Dodoma. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akikata utepe kuzindua Ujenzi wa Kanisa Kuu la Africa Inland Church Tanzania Dayosisi mpya ya kanda ya kati Dodoma. Askofu Mteule Amos Katoto Ngeze mara baada ya kuwekwa Wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa kwanza wa kanisa la African Inland Church wa kanda ya Dayosisi ya kati Dodoma. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa t...

TATHMINI YA WATOTO DAR

Image
Wajumbe wa PJT -MMMAM wa Mkoa wa Dar es Salam wakiwa kwenye picha ya pamoja  Na PATRICIA KIMELEMETA KATIBU Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar Es Salaam ambaye anashughulikia Ufuatiliaji,Menejimenti na Ukaguzi, Saloni Nyika, amewataka watendaji wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanatekeleza kwa vitendo afua tano za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili waweze watoto hao waweze kukuza katika hali ya utimilifu. Hayo yamejili baada ya Serikali kuzindua Programs Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kuanzia umri 0 hadi miaka minane ambayo inatekelezwa kwa muda wa miaka mitano ambapo ilianza 2021 hadi 2026. Programu hii ina afua tano ambazo kila Halmashauri kwa kushirikiana na Asasi za kiraia, wanapaswa kuzitekeleza kwa vitendo ambazo ni pamoja na afya, elimu, lishe, Malezi yenye mwitikio, ulinzi na Usalama. Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa programu hiyo, Nyika alisema kuwa usimamizi wa Malezi katika jamii ni jambo la muhimu na l...

KINANA AWAAMBIA VIJANA SOMENI SERA, ILANI ,KANUNI,KATIBA NA MWELEKEO WA CHAMA

Image
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulhaman Kinana, akiwasili katika ukumbi  wa Mikutano wa Jiji la Dodoma (Mitumba)kwa ajili ya kufungua Mkutano wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho unaofanyika leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo na kulia ni Katibu Mkuu UVCCM, Kenani Kihongosi. . amewataka vijana kusoma sana na kukielewa chama nini kinataka na muwaelewesha washindani wenu  ikiwa ni njkia ya kujenga nchi . Mkutano huo mkuu wa uchaguzi umehudhuliwa na vyama marafiki wa CCM, wakitokea umoja wa vijana wa vyama tawala, Msumbiji, Afrika Kusini, Burundi na Zimbabwe na vyama vya Siasa nchini  vya CUF  na NCCR-Mageuzi. Wajumbe wa Mkutano huo wakimashangilia Ktibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha ANC, alipokuwa akizungumza akitema madini kuhusu kujikomboa kwa Waafrika kujiepusha na wakoloni. na kutana kiswahili kiwe ndiyo lugha sasa ya mawasiliano. Chongolo akizunguza