KITUO CHA MICHEZO KUKIZINDUA JK
PROFESA KIKWETE MGENI RASMI UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO Na Mwandishi wetu_MAELEZO-Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha michezo katika eneo la Kidongo Chekundi jijini Dar es salaam. Kituo cha michezo kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali ya Tanzania. Shehere hizo zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi. Kwa mijbu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na uzind...