TUTAWAPIGANIA VIJANA WOTE WA CHADEMA NA TUTAWASOMESHA POPOTE NDANI YA NCHI AU NJE YA NCHI---HECHE
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amewataka vijana wa chama hicho kupitia Baraza lao la BAVICHA kukipigiania chama hicho kwa lolote popote na wasiwe na woga, wao kama viongozi watawatetea popote watakapokutwa na madhira yoyote na hawatawatelekeza. Heche aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Vijana Duniani kwa vijana wa chama hicho lililofanyika jijini Dodoma, amebainisha kwamba vijana wa chama hicho waliokamatwa huko Geita wakisingiziwa kesi za Ugaidi watawatetea na wale wanafunzi pindi kesi zao zikiisha watawalejesha shuleni na watasoma popote pale Duniani. 
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Deogratius Mahinyila, akizungumza katika mkutano huo Kabla ya kumruhusu Heche kuzungumza
Lema, akitema cheche katika kongamano hilo
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Mwambukusi, akihutubia kongamano hilo na kuwataka vijana wa chama hicho kutochoka kudai haki na katiba bora
Wakisikiliza kwa makini
Mwanaharakati Deus Kibamba, akihutubia Kongamano hilo akiwataka Vijana kuwa ngangari kudai haki na katiba bora siyo mchezo wawaulize wenzao wa nchi zilizokomborewa na Tanzania chini ya Mwalimu Nyerere ilikuwaje, watume ujumbe hata nje ya nchi siyo kulalamikia hapa tuu

Comments
Post a Comment