TANZANIA YA TATU KWA UBORA WA MBEGU AFRIKA
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ndugu Nyasebwa Chimagu, akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma leo ,kuhusu huduma za mbegu zinazotolewa na Taasisi yake, Kwa Twakimu za Kimataifa Mkurugenzi huyo alisema Tanzania ni ya tatu kwa ubora wa mbegu barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini na Nigeria na Kidunia ni ya 15, Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kwamba Mbegu ni bidhaa inayosimamiwa na
Serikali (regulated product) duniani kote kutokana na umuhimu wake
kwa usalama wa chakula na lishe, na ni mojawapo ya pembejeo muhimu
katika kuleta mageuzi ya kilimo (Agricultural Transformation) kwa
kuongeza tija au technical efficiency, mapato na ubora wa mazao.
Aidha, biashara ya mbegu hufanyika pia kimataifa kwa kuzingatia
viwango vya ubora vya kimataifa. Mathani, hadi mwaka 2026, thamani
ya biashara ya mbegu duniani ilifikia Dola za Kimarekani Bilioni 67.2.
Kutokana na umuhimu huo, nchi nyingi duniani zina taasisi mahiri kwa
ajili ya kusimamia tasnia ya mbegu hususan kuanzia hatua ya utafiti,
uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mbegu bora.
Hapa Tanzania Taasisi yenye jukumu hilo ni Taasisi ya Kuthibiti Ubora
wa Mbegu Tanzania (TOSCI) iliyo chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa
kwa Sheria ya Mbegu Sura ya 308 (Toleo la Urekebu 2023) au inaweza
kurejewa kama Sheria ya Mbegu Na.18 ya mwaka 2003.
1
Umuhimu wa mbegu bora:
Chanzo cha usalama wa chakula na ustawi wa mazao
Kuongezeka kwa tija
Kinga dhidi ya visumbufu vya mazao na mabadiliko ya tabianchi
Ajira katika mashamba ya mbegu, viwanda vya kuchakata mbegu,
maduka ya kuuza mbegu na usafirishaji
Kuaminika kimataifa katika biashara ya mbegu ikiwa ni sehemu ya
kuingiza fedha za kigeni
2. BAJETI YA WIZARA YA KILIMO
Ndugu Waandishi wa Habari, tunapokutana leo hapa kueleza
mafanikio katika tasnia ya mbegu, hatuwezi kuacha kusema kwa ujasiri
namna Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoamua kuipa kipaumbele sekta ya
kilimo ikiwa ni sekta ya uzalishaji inayoajiri watanzania wengi
ikijumuisha tasnia ya mbegu. Kuwa na kipaumbele ni suala moja
muhimu lakini kutoa rasilimali za uwekezaji na kusimamia utekelezaji ni
suala muhimu zaidi. Katika kipindi cha miaka mitano sasa uongozi wa
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania (Mhula wa Kwanza na Mhula wa Pili unaoendelea),
Serikali imeendelea kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa ajili ya
uwekezaji unaowezesha sekta ya kilimo kutoa mchango unaostahili
katika uchumi kwa kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza ajira,
upatikanaji wa malighafi za viwanda na kukidhi mahitaji ya masoko ya
ndani na kimataifa.
i.
Bajeti ya kilimo imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 294 mwaka
2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 751 mwaka 2022/2023 sawa na
ongezeko la asilimia 155;
2
ii.
Kadhalika, Bajeti imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 751 mwaka
2022/2023 hadi Shilingi Bilioni 970 mwaka 2023/2024 sawa na
ongezeko la asilimia 29.2;
iii.
Vilevile, kutoka Shilingi Bilioni 970 mwaka 2023/2024 hadi Trilioni
1.248 mwaka 2024/2025; ambayo imeendelea kwa kiwango hicho
hadi mwaka 2026/2027.
Maeneo ya kipaumbele katika uwekezaji huo ni ujenzi wa
miundombinu ya umwagiliaji, ghala, kuimarisha utafiti, uzalishaji wa
mbegu bora na huduma za ugani.
Ndugu Waandishi wa Habari, kati ya maeneo hayo ya kipaumbele
kwenye sekta ya Kilimo ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameyapa kipaumbele na
kuwapa dhamana viongozi wakuu wa Wizara ya Kilimo Mheshimiwa
Daniel Godfrey Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo na Bw. Gerald G. Mweli,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Leo hii kupitia ninyi wandishi wa Habari kwa niaba ya Serikali ninapenda
kuwahabarisha Watanzania kuhusu mafanikio katika tasnia ya mbegu
kwa mwaka 2025/2026 na mwelekeo kwa mwaka 2026/2027 chini ya
Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ninayoiongoza
kama Mkurugenzi Mkuu.
3. MAFANIKIO KATIKA TASNIA YA MBEGU
i.
Bajeti katika Tasnia ya Mbegu
Ndugu Wandishi wa Habari, Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti
katika tasnia ya mbegu inayojumuisha utafiti, uboreshaji wa miundombinu
ya uzalishaji na uthibiti wa ubora kutoka Shilingi Blioni 16.79 mwaka
2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 85.15 sawa na ongezeko la asilimia 307;
3
ii.
Uzalishaji wa mbegu zilizothibitishwa ubora na TOSCI
Ndugu Wandishi wa Habari, katika mpango wa kijitegemea kwa mbegu,
uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo umeongezeka kutoka tani
50,750 mwaka 2021/2022 hadi tani 78,842 mwaka 2025/2026 sawa na
ongezeko la asilimia 55.35. Kati ya hizo, tani 45,101 za mbegu bora sawa
na asilimia 57.2 zimezalishwa hapa nchini kupitia Wakala wa Mbegu za
Kilimo (ASA) na Makampuni binafsi, na tani 33,741 (42.8%) zimeagizwa
kutoka nje ya nchi.
iii.
Ruzuku ya mbegu za mahindi
Kwa upande wa ruzuku ya mbegu bora za mahindi zilizothibitishwa na
TOSCI, jumla ya tani 42,850.19 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 333.28
zimeuzwa kwa wakulima katika mikoa yote nchini. Kati ya fedha hizo,
Shilingi Bilioni 68.75 ni ruzuku ya Serikali na Shilingi Bilioni 264.54 ni
mchango wa wakulima.
Uzalishaji huu wa mbegu uchangia kuifaya Tanzania kuendelea
kujitegemea kwa chakula kwa utoshelevu wa asilimia 130 kwa
kuzalisha tani 23,783,128 za chakula kwa msimu wa 2024/2025 na
kuwa na ziada ya tani 5,504,074. Kwa zao la mahindi, nchi yetu
ilizalisha tani 10,925,025 na kuwa ya tatu barani Afrika kwa uzalishaji
wa mbegu za mahindi baada ya Afrika Kusini na Nigeria.
Aidha, kwa mujibu wa takwimu za USDA, kwa msimu wa 2025/2026
Tanzania ilishika nafasi ya 10 kwa kuwa na eneo la kilimo cha
mahindi la Hekta Milioni 4 ikitanguliwa na China (Hekta Milioni 45),
Marekani Hekta Milioni 36.9 na Brazili Hekta Milioni 22.8).
Tumeendela kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi kama vile mahindi,
mchele, mazao ya jamii ya mikunde na horticulture kutokana na
kuzingatia kilimo biashara ikiwemo matumizi ya mbegu bora.
4
iv.
Ujenzi wa Maabara za Mbegu na Vifaa vya Maabara
Ndugu Waandishi wa habari, maabara ni mojawapo ya miundombinu
muhimu katika uthibiti wa ubora wa mbegu kwa kupima viwango vya
ubora kama vile uhalisia (purity), uotaji (germination), upimaji wa
unyevu, afya ya mbegu (seed health), na vipimo vingine vya bayokemia
(protin, mafuta, sukari, madini), vipimo vya viinilishe (vutamin, Zinc,
Chuma, Calcium), GMO, mabaki ya kemikali, aina ya nasaba za ubora wa
mbegu.
Katika mwaka 2025/2026 Serikali itoa fedha kuimarisha uwezo wa
TOSCI katika uthibiti ubora wa mbegu kwa viwango vya kimataifa
ikizingatiwa kuwa TOSCI ina maabara ya taifa ya mbegu yenye ithibati
ya kimataifa ya ISTA. Utekelezaji ni ifuatavyo:-
MAHALI
JINA
Na.
MRADI
LA
MRADI
UNAKOTEKELEZWA
THAMANI YA
FEDHA
(SHILINGI)
HATUA ILIYOFIKIWA
YA UTEKELEZAJI
1
Ukarabati
wa Maabara
ya
Kisasa
ya Taifa ya
Mbegu
1,838,956,142
Ujenzi wa Maabara ya
Taifa
ya
Mbegu
Morogoro
Ujenzi
wa
Maabara ya
Kisasa
2
na
Ofisi Kanda
ya Kusini –
Mtwara:
Mtwara
1,220,173,378
Morogoro
asilimia 99.
Mradi
umefikia
ulisainiwa
tarehe 22 Mei, 2026,
ujenzi
umeanza
mwezi Juni, 2026 na
kutarajiwa kukamilika
Februari 2027
Ujenzi
3
wa
Maabara ya
Kisasa
na
Ofisi Kanda
Mradi
1,203,032,639
Nzega, Tabora
umeanza
mwezi Juni, 2026 na
ulisainiwa
tarehe 22 Mei, 2026,
ujenzi
5
MAHALI
LA
Na.
JINA
MRADI
THAMANI YA
FEDHA
(SHILINGI)
MRADI
UNAKOTEKELEZWA
HATUA ILIYOFIKIWA
YA UTEKELEZAJI
ya
Magharibi
Tabora
Ujenzi
kutarajiwa kukamilika
Februari 2027
Mradi
wa
Maabara ya
Kisasa
4
na
Ofisi Kanda
ya Ziwa –
Mwanza
ulisainiwa
tarehe 22 Mei, 2026,
ujenzi
1,208,999,116
Mwanza
5
Uboreshaji
wa huduma
za maabara
kwa
vitendea
kazi
1,762,597,000
umeanza
mwezi Juni, 2026 na
kutarajiwa kukamilika
Februari 2027
Vifaa
vya
ya kipima sifa
mahsusindani na nje
ya mbegu.
Jumla ndogo ya Fedha kwa Miradi Yote ya Ujenzi 2025/2026 –TZS 7,233,758,275
Makao Makuu na Mbaara
za Kanda
v. Usajili wa aina mpya za mbegu
kisasa
vimenunuliwa ikiwemo
germination chambers
kwa ajili ya majaribio
ya uotaji, fume hoods
kwa ajili ya kijikinga
na kemikali hatarishi,
seed analyser kwa
ajili
Ndugu waandishi wa Habari, ili mbegu iweze kuzalishwa na kuuzwa
hapa nchini au nje ya nchi, Sheria inataka ni lazima iwe imekidhi vigezo
6
muhimu ikiwemo kusajiliwa baada ya majaribio ya kufaa kwa uzalishaji
kwa mazingira ya Tanzania na pia iwe ni teknolojia mpya.
Katika mwaka 2025/2026 Wizara ya Kilimo kupitia TOSCI ilisajili aina
mya za mbegu 113 za mazao mbalimbali baada ya kukamilika kwa utafiti
na kukidhi viwango. Mchanganuo wa aina mpya zilizosajiliwa kwa
mwaka 2025/2026 ni zifuatazo:-
a) Mahindi aina 6;
b) Mtama aina 2;
c) Mharage ya soya aina 1;
d) Muhogo aina 2;
e) Tumbaku aina 3;
f) Ndizi aina 12;
g) Alizeti aina 2;
h) Parachichi aina 5 (HASS, PINKERTON, FUERTE, X-IKULU na
BOOTH 7);
i) Mazao ya bustati (horticulture) aina 85
Usajili huo unafanya jumla aina mpya za mbegu 1318 zilizosajiliwa hapa
nchini zikiwemo za mahindi aina 229, ngano aina 31, mtama aina 25,
mpunga aina 27, maharage aina 58, soya aina 12, alizeti aina 19, ufuta
aina 5, pamba aina 8, MALISHO 9, na korosho aina 64.
Tunaendelea kusisitiza watafiti kugundua aina mpya za mbegu
zinazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya nchi, changamoto za
uzalishaji, mahitaji ya wakulima na soko. Mathani kweye korosho tuna
aina 64 za mbegu za korosho zinazoweza kuzalishwa katika mikoa
mbalimbali zaidi ya mikoa iliyozoeleka ya Mtwara na Lindi. Leo hii
7
Korosho inazalishwa Dodoma, Singida, Morogoro, Tanga, Mbeya na
mikoa mingine hali inayoifanya Tanzania kuongeza uzalishaji na kuwa
katika ramani ya Dunia. Uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani
210,786.80 mwaka 2020/2021 hadi tani 618,497.41 mwaka 2025/2026
na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa 4 duniani baada ya Ivory Coast
(Tani 1,5000,000), Cambodia (tani 1,020,000), na India tani 750,000.
vi.
Udhibiti wa matukio ya mbegu zisizokidhi viwango vya
ubora (mbegu feki)
Ndugu Waandishi wa Habari, Wizara ya Kilimo kupitia TOSCI
imeendelea kudhibiti matukio ya mbegu zisizokidhi viwango vya ubora
kwa kuimarisha ukaguzi wa maduka ya mbegu, ghala na viwanda vya
kuchakata mbegu kwa kushirikiana na Uongozi wa Ofisi za Waheshimiwa
Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na vyombo vya ulinzi na
usalama. Kutokana na hatua hizo katika mwaka 2025/2026 wahusika wa
matukio ya ukiukwaji wa Sheria ya Mbegu wapatao 22 wamechukuliwa
hatua mbalimbali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani, kulipa
faini na fidia kwa wakulima.
4. MAENEO MENGINE YA MAFANIKIO KATIKA TASNIA YA MBEGU
i.
Viashiria vya Ufanisi katika Tasnia ya Mbegu
Ndugu Waandishi wa Habari, Tanzania inashika nafasi ya 3 kati ya
nchi 55 za Umoja wa Afrika (AU) ikiwa na wastani wa alama 7.25 kati ya
10 kwa ubora wa Sekta ya Mbegu baada ya Afrika Kusini (8.62) na
Zambia 7.89 (The African Seed Access Index – TASAI, 2023)
Maeneo yaliyofanya vizuri: ubora wa vifungashio vya mbegu (9.89),
Sheria na Sera za Mbegu (9.00), Mifumo ya Mbegu inayosimamiwa na
Wakulima (9.00), Kuoanisha Sheria na Sera za Mbegu na Miongozo ya
8
Kikanda (8.00), Mfumo wa uidhinishaji aina mpya za mbegu (8.00),
taratibu za kuuza mbegu nje na kuingiza mbegu ndani ya nchi (8.00),
uwepo wa kutosha wa mawakala wa mbegu (8.00), na udhibiti wa
mbegu ambazo hazikidhi viwango (8.00)
ii.
iii.
Ithibati ya International Seed Testing Association (ISTA)
Ndugu Waandishi wa Habari, kwa mwaka 2025/2026 Tanzania
imeendelea kudumisha uanachama wake kwa ISTA. Aidha,
Tanzania ni miongoni mwa nchi 14 za Afrika na 80 duniani zenye
maabara zilizo na Ithibati ya kimataifa ISTA. Faida ya ithibati ya
ISTA ni Tanzania kutambuliwa kimataifa katika umahiri wa
kitaalamu wa upimaji wa ubora wa Mbegu, kutoa vyeti vya (ISTA
Orange
International
Certificate -OIC)
kwa
Mbegu
zinazosafirishwa nje ya nchi; na kuvutia wawekezaji wapya wa
biashara ya mbegu kimataifa. Tunazo kampuni za kimataifa
(multinational companies) takriban 29 zinazohusika
katika uzalishaji na biashara ya mbegu hapa nchini.
Uanachama wa Skimu za Mbegu za OECD
Ndugu Waandishi wa Habari, Tanzania ni miongoni mwa nchi
10 za Afrika zinazoshiriki katika skimu za mbegu za kimataifa za
Shirika la OECD na kwa mwaka 2025/2026 tumeendelea
kudumisha uanachama.
Umuhimu wa Tanzania kuendelea kulinda uanachama wake kwa
kuimarisha maeneo yote muhimu ikiwemo kuwa na maabara bora
utachangia katika kukuza ushirikiano wa Kimataifa na bidhaa za
mbegu kuuzwa bila vikwazo vya kimasoko.
Mathani, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, jumla ya vibali 392
vimetolewa kwa ajili ya kuuza nje ya nchi tani 993.21 za mbegu.
Kati ya hizo, tani 55.44 zilikuwa mbegu za mazao ya bustani, tani
9
204.07 za nafaka, tani 722.2 za mikunde na tani 11.5 za mazao ya
mafuta.
5. MWELEKEO KWA MWAKA 2026/2027
Ndugu Waandishi wa Habari, sote tunatambua kuwa tarehe 17 Julai,
2025 jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan, alizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwa ni
Ramani ya Tanzania tuitakayo ifikapo mwaka 2050. Katika uzinduzi
huo, pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais alielekeza “Kila taasisi ya
Serikali italazimika kuwa na vigezo vya kupima utendaji (Key Performance
Indicators – KPIs) vinavyoendana na malengo na shabaha ya Dira,”. Aidha,
tarehe 03 Agosti, 2026 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
alizundua nyenzo za utekelezaji wa Dira jijini Dar es Salaam.
Hivyo basi, kwa kuzingatia maelekezo hayo ya Mheshimiwa Rais, Shabaha
za Dira 20250 sambamba na Mpango Kabambe wa Mageuzi katika Kilimo
kwa Mwaka 2026/2026 Wizara ya Kilimo kupitia TOSCI inaendelea na
utekelezaji wa malengo na Shabaha za Dira kwa kutekeleza yafuatayo:-
i.
Kuwezesha uwekezaji na biashara ya mbegu kwa kuimarisha
uratibu wa wadau na uthibiti ubora kwa mazao ya kipaumbele
ambayo ni pamoja na mazao ya mboga mboga, matunda na
viungo; pamba, korosho, mkonge, kahawa, mahindi, ufuta, alizeti,
mpunga, ngano, mtama, maharage ya soya, mazao ya jamii
yamikundi, na malisho ili kufungamanisha sekta ya kilimo mazao
na ufugaji. Hatua hizi zinafanywa kwa kuzingatia kuwa mojawapo
ya shabaha za Dira ni kuifanya Tanzanua kuwa mzalishaji mkubwa
wa Chakula barani Afrika na miongoni mwa nchi 10 duniani ifikapo
mwaka 20250;
Tutaimarisha mafunzo kwa wadau ili waweze kuzalisha
mbegu za mazao ya kipaumbele kwa viwango
vinavyokubalika
Tushirikiana na sekta binafsi na sekta ya umma kuvutia
mitaji ya kuwekeza katika sekta ya mbegu kupitia
10
majadiliano kwa manufaa ya wote na kutengeneza sera za
utoaji wa mitaji katika tasnia ya mbegu
Kutumia miundombinu iliyopo kutoa mafunzo kwa wanafunzi
na wahitimu kwenye vyuo vya elimu ya juu kama sehemu
ya Elimu Amali kuwapatia ujuzi katika tasnia ya mbegu ili
waweze kujiajiri hususan vijana na wanawake
Kushirikiana na Uongozi wa Mikoa na Wilaya katika kutenga
na kulinda ardhi kwa ajili ya mashamba ya mbegu ili
kuondoa utegemezi wa kuagiza kutoka nje.
ii.
iii.
iv.
v.
vi.
Kuendelea kusimamia kamilishaji wa miradi ya maendeleo ya
maabara mpya katika mikoa ya Mwanza, Tanora na Mtwara; na
Arusha.
Kuundelea kununua na kusimika vifaa vya kisasa vya maabara za
mbegu.
Kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora tani 105,000
zilizothibitishwa ubora kwa wakulima kulingana na Kalenda ya
kilimo sambamba na kudhibiti mbegu feki kwa watu wenye nia
ovu.
Uimarishaji wa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za
uthibiti wa ubora wa mbegu. Hivi karibuni tutakamilisha
maboresho ya Mfumo wa TEHAMA wa TOAS.
Kuendelea kuimarisha mashirikiano ya kikanda na kimataifa ili
kubadilishana maarifa, uzoefu, teknolojia na kuoainisha viwango
vya ubora.
6. HITIMISHO
Ndugu Waandishi wa Habari, Mbegu bora itaendelea kuwa nguzo
muhimu ya kuleta mageuzi ya kilimo kama walivyofanikiwa mataifa
mengine kwa kuwa mbegu ni uhai, mbegu ni biashara na mbegu bora
inalipa.
Ndugu Waandishi wa Habari, nihitimishe kwa kuwashukuru nyote
kwa kufika katika mkutano huu ili kuwahabarisha watanzania. Aidha,
11
niwashukuru wote ambao wamefuatia mkutano huu kwa njia mbalimbali
ya vyombo vya habari. Aidha, nishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo kwa kuandaa na kuratibu Mkutano huu.
Nichukue nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Daniel Godfrey Chongolo
(Mb), Waziri wa Kilimo na Bw. Gerald G. Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Kilimo kwa kuendelea kusimamia vipaumbele vya Taifa vya
kuendeleza sekta ya kilimo hususan eneo la tasnia ya mbegu ambayo
TOSCI imepewa dhamana ya kuisamia kwa mujibu wa Sheria ya Mbegu
Sura ya 308 (Toleo la Urekebu 2023).
Kipekee nimshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kama nilivyoeleza awali
amekuwa kinara wa kuleta mageuzi katika kilimo na kuamusha fikra za
kilimo biashara kwa makundi mbalimbali ya watanzania kutoka na
uwekezaji anaoufanya kwenye kilimo ikiwemo fedha za utafiti, uzalishaji
na uthibiti wa ubora wa Mbegu sambamba na kufungua masoko. Hatua
hizo zimedhihirisha Tanzania itafikia malengo yake ya kuilisha dunia
ikiwa ni moja ya Shabaha za Dira ya 20250.
Wanahabari wakiwajibika
Wanahabari wakiwajibika
Comments
Post a Comment