KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE LAAC YATOA MAELEKEZO KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Ado Shaibu, ameongoza kikao cha kamati yake na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Same, ambapo walikaa na kupitia hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.Mwenyekiti huyo akisoma tamko la kamati amewataka viongozi hao kutekeleza maagizo yote ya Mkaguzi na yale yanayotolewa na Kamati yake , aidha amewarudisha kwenda kutekeleza na watawaita tena kujiridhisha kama maagizo hayo yote yametekelezwa kama kamati hiyo ilivyoagiza. Aidha ametoa onyo kwa Halmashauri zote nchini kutekeleza maagizo yanayotolewa na Mkaguzi Mkuu na Kamati yake, amefafanua kwamba kamati hiyo inapoziita Halmashauri ifahamike kwamba kamati yake inafanya kazi kwa niaba ya bunge kuidharau kamati hiyo ni kulidhalau bunge kitu ambacho hakubaliki hata kidogo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Jimson Mhagama (kushoto), akiwaongoza watendaji wake kuingia katika chumba cha mikutano cha Kamati ya Kudumu ya Bunge LAAC kusikiliza shauri lao, hata hivyo wamekutwa na kosa la kutotekeleza maagizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali na za Kamati hiyo

Comments
Post a Comment