JWT MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA SITA YA WIKI YA USHIRIKIANO KWA MAJESHI YA EAC

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Utawala wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Brigedia Jenerali Agatha Mary Katua, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo kuhusu maadhimisho ya sita ya majeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotalajiwa kuanza Agost 26 2026. Katua alisema kwamba Jwtz ni mwenyeji  wa Maadhisho hayo kwa nchi za Afrika Mashariki (The 6th EAC Amerd Forces Civilian Military Co-operation Week),  maadhimisho hayo yatafanyika sehemu mbalimbali za nchi hii.

 Maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa wanachama kwa kupokezana ambapo kwa mara ya mwisho kufanyika hapa nchini ilikuwa mwaka  2022.

Aidha, katika kuadhimisha Ushirikiano huo , Majeshi ya nchi  Wanachama hutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu ambapo Madaktari Bingwa kutoka Burundi, Somaria, Tanzania, Rwanda, Kenya na Uganda yatatoa huduma hiyo katika hospitali na vituo vya afya.

Sambamba na huduma za tiba , kutakuwa na utoaji wa misaada ya kijamii, ukarabati  wa vituo vya afya na vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na Magereza. Huduma hizo zitatolewa katika mikoa ya Dar es Salaa, Pwani , Arusha na Zanzibar ambapo kwa upande wa Dar es Salaam vituo vitakavyotumika ni Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Hospitali ya Vijibweni Kigamboni na Kituo cha afya Yombo Malawi. Kwa upande wa Mkoa wa Pwani ni Hospitali Teule ya Rufaa ya  Tumbi na Hospitali ya Wilaya  Bagamoyo. Kwa upande wa Zanzibar huduma zitatolewa kwenye Hospitali ya Wilaya ya MweraPongwe Unguja na Hospitali ya Wilaya ya Vitongojini Pemba.

Mkurugenzi huyo alisema kwa upande wa vituo vya Watoto Yatima  ni pamoja na Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini- Temeke Kituo cha Mwandaiwa Orphanage Centre -Bunju-Kinondoni, Kituo cha Chanika Children Shelter- Ilala na SOS Orphanage Centre Zanzibar. Pia utafanyika ukarabati wa Majengo katika Kituo cha Makao ya Taifa ya watoto Kurasini -Temeke Kituo cha Afya Mapinduzi Dpdpma- Chamwino na Kituo cha Afya Kibokoni Pemba. Kwa upande wa Misaada kwa Wafungwa huduma hiyo itatolewa katika Gereza la Segerea-Dar es Salaam na Gereza la Kisongo Arusha.




Wanahabari wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi huyo




 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA