KAMATI YA KISWAGA YAPOKEA MAONI YA GGGI JIJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maji na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karenga Jackson Kiswaga, akifungua kikao cha maoni ya wadau wa Maji na mazingira kuhusu Mkataba wa Global Green Growth Institute (GGGI) kilichofanyika leo jijini Dodoma, ambapo mada mbalibali ziliwasilishwa na maoni ya wadau hao kabla haujapelekwa kwa spika na kuingizwa bungeni kwa ajili ya maoni ya wabunge. Kamati hiyo ilibainisha kwamba Taasisi ya Global Green Growth Institute (GGGI) ni Taasisi ya Kimataifa ambayo inajihusisha na maendeleo ya dunia, katika kusaidia na kukuza uchumi imara shirikishi na endelevu kwa wananchama wake. Aidha wabunge walibainishiwa kwamba Wanachama wa Taasisi hiyo ni pamoja na nchi zilizoendelea na zinazoibukia kiuchumi ambazo ni mwananchama wa Umoja wa Mataifa na Jumuia za Kikanda.

Taasisi hiyo ilianzishwa kupitia mkataba wa kimataifa ulioidhinishwa (adopt) katika jiji la Reo de janeiro, Brazil Juni 12, 2012. Mmoja ya wasilisho katika  mada ilisema kuwa mkataba huo ukilidhiwa utakuwa na manufaa kama, kuimalisha kwa uwezo wa kuibua na kuandaa miradi ya uhifadhi na usimamizi wa  mazingira na mabadiliko ya tabia nchi; kuongezeka kwa taasisi za ndani zenye ithibati katika usimamizi wa fedha za kukabiliana na tabianchi; kuongezeka kwa fedha za misaada na mikopo nafuu kwa nchi; kuimarika kwa mbinu za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi kupitia tafiti na  kuongezeka kwa tija na uzoefu wa wataalamu wa ndani katika masuala ya ukuaji wa uchumi wa kijani.



Wajumbe wa Kamati hiyo wakisikiliza wawasilisha mada kwa umakini mkubwa







Watoa maoni wakitoka zao mkutanoni

 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA