WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA 88 JKT KUJIONEA MAAJABU YAO
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (aliyeshika chupa ya asali), leo ametembelea Maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma, na kulipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa bidhaa zake bora zinazozalishwa katika vitengo mbali mbali, akizungumza baada ya kumaliza ziara yake na kusema ameweza kujionea uzalishaji wa asali ambayo yeye anaipenda sana, uzalishaji wa kisasa kwa maji ya kunywa Pamoja na drip za mahospitalini, viatu vya kijeshi na kilaia nguo kama yunifumu za majeshi mbalimbali. amewataka vijana wanaoenda kujiunga na jeshi hilo kujifunza ujuzi huo kisha waludipo uraiani waje wajitegemee hizo ndizo ajira badala ya kukazania ajira serikalini. " Hili ndilo jeshi linalohitajika kwa vijana wanapojiunga nalo waludipo majumnani waende wakajiajili kama, ufugaji wa Samaki, kuku wa mayai ,utengenezaji wa sabuni ,ufugaji wa nyuki, utengenezaji wa finicha, na ukulima wa kisasa nawapongezeni sana. Pia wananchi nawaomba watembelee JKT wajionee wenyewe wasingoje kusimuliwa",alisema Pinda
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa wa JKT ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Suma JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, alimweleza Waziri Mkuu Mstaafu Pinda kwamba hivi sasa wamefunga mtambo mpya wa kutegeneza maji ya kunywa na wanatengeneza hata maji ya Mahospitalini (Drip Water), hivyo hivyo kwa upande wa utegenezaji wa yunifomu za majeshi yote nchini Pamoja na viatu vyake, Shija alimhakikishia Pinda kwamba jeshi hilo linatengeneza bidhaa nyingi ambapo sasa makampuni yaje kununua kwao badala ya kwenda kununua nje ya nchi. Msikiliza Pinda katika Mhagale Online Tv anavyolizungumzia jeshi hilo la kisasa.Akiangalia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi hilo

Mwenyekiti wa
Kamati ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa wa JKT ambaye pia ni Naibu
Mkurugenzi wa Suma JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi (kulia), akimfafanulia jambo PindaNaye Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa wa JKT ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Suma JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, alimweleza Waziri Mkuu Mstaafu Pinda kwamba hivi sasa wamefunga mtambo mpya wa kutegeneza maji ya kunywa na wanatengeneza hata maji ya Mahospitalini (Drip Water), hivyo hivyo kwa upande wa utegenezaji wa yunifomu za majeshi yote nchini Pamoja na viatu vyake, Shija alimhakikishia Pinda kwamba jeshi hilo linatengeneza bidhaa nyingi ambapo sasa makampuni yaje kununua kwao badala ya kwenda kununua nje ya nchi. Msikiliza Pinda katika Mhagale Online Tv anavyolizungumzia jeshi hilo la kisasa.Akiangalia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi hilo
Akiangalia asabuni Akiangalia batikiakiangalia miguu bandia inayotengenezwa na Jeshi hilo
Akiangalia meza ya chakula iliyotengenezwa na kiwanda cha jeshi hilo cha Chang'ombe jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa wa JKT ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Suma JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, akimweleza jambo Waziri Mkuu Mstaafu Pinda
Comments
Post a Comment