WAKULIMA TANZANIA CHANGAMKIENI MIKOPO KWENYE BENKI YAKE---NYABUNDEGE

 

Mkurugenzi Mwendeshaji,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege, akizungumza na wanahabri leo asubuhi katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Mtumba jijini Dodoma, Mkurugenzi  huyo, amewaomba wakulima wa tanzania kuchangamkia mikopo inayotolewa na benki hiyo ambayo liba yake ni kidogo, akawataka wajiepushe na mikopo ya kausha damu ambayo imekuwa ikiwafanya wananchi kudaiwa na wengine kupata presha na kupelekea vifo. Aidha alianza kuwaeleza wanahabri kwamba
 
TADB ni benki ya Serikali iliyoanzishwa kuwezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kupata huduma za kifedha.
•    Adhima kuu ya TADB ni kuchangia kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini kupitia mageuzi ya sekta ya kilimo.
•    TADB inatekeleza dhamira hiyo kwa kutoa suluhisho bunifu za kifedha zinazojenga minyororo ya thamani ya kilimo iliyo endelevu na jumuishi.
•    Benki imeanzishwa pia kuhakikisha kilimo kinabadilika kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara chenye tija na ushindani.

2.    SHUKRANI KWA MHESHIMIWA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUIMARISHA MTAJI WA TADB

•    Namshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yaliyoifanya TADB kukua na kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
•    Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mtaji wa Benki na kuongeza uwezo wake wa kuhudumia sekta ya kilimo.

Ukuaji wa mtaji wa TADB:
•    Kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa Benki ulikuwa shilingi bilioni 60.
•    Mwaka 2021: Serikali iliongeza mtaji wa shilingi bilioni 208, na kufanya mtaji kufikia shilingi bilioni 268.
•    Mwaka 2024: Serikali iliongeza mtaji kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wenye thamani ya shilingi bilioni 174.16, na kufanya mtaji kufikia shilingi bilioni 442.16.
•    Mwaka 2025: Serikali iliongeza mtaji kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa shilingi bilioni 10, na kufanya mtaji kufikia shilingi bilioni 452.16.

3.    NAFASI YA SERIKALI KATIKA BENKI YA TADB: MTAJI WA SASA WA BENKI NA MCHANGO WA FEDHA ZA WAFADHILI KATIKA KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Mafanikio Katika Utafutaji wa Fedha 
S/N    Aina ya Fedha    Kiasi (TZS Billion)
1    Mtaji Kutoka Serikalini    452.16
2    Mikopo kutoka Washirika Maendeleo – AFD (2022) & JICA (2025 )    445.6.
3    Mfuko wa Dhamana (SCGS) – IFAD (2018) & AFD (2022)     108.4
4    Fedha zinazosimamiwa kwa niaba ya serikali (Managed Funds)      36.54

4.    VIPAUMBELE VYA TADB UKIOANISHA NA MPANGO WA MAENDELEO 2050
 

5.    TREND YA MIAKA 5 YA PERFORMANCE YA BENK KATIKA MIKOPO YA MOJA KWA MOJA NA SGCS
 
•    73.6% ya mikopo ya benki imetolewa katika ya mwaka 2022 hadi 2025 wakati wa uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 
6.    TIJA ILIYOPATIKANA BAADA YA KUTOA MIKOPO NA TADB

 7.    MIKAKATI YA BENKI
Ndugu Wanahabari, Mabibi na Mabwana; 

Kwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele ya TADB, mikakati yetu kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni:

•    Kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo, na uvuvi. 
•    Kuimarisha mnyororo wa thamani ya kimkakati ili kuongeza mauzo nje ya nchi na kupunguza utegemezi kutoka nchi za nje. 
•    Kukuza kilimo cha kisasa na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija na ushindani. 
•    Kuwezesha vijana na wanawake kupata huduma za kifedha na kushiriki kikamilifu katika biashara za kilimo. 
•    Kukuza kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi kwa kufadhili teknolojia na miradi endelevu. 
•    Kuimarisha ushirikiano na Serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kuongeza rasilimali za uwekezaji. 
•    Kuchochea uongezaji thamani na mauzo ya bidhaa za kilimo ndani na nje ya nchi, hivyo kuchangia ajenda ya uchumi wa viwanda na diplomasia ya uchumi.

Hitimisho

Ndugu Wanahabari,Mabibi na Mabwana;

TADB itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuimarisha sekta kilimo-mazao, mifugo na uvuvi kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Aidha, kama mnavyojua sasa ni msimu wa 88 NA kutokana na umuhimu wa Maonesho ya Nane Nane katika kukuza sekta ya kilimo, TADB inaendelea kuyaunga mkono kwa kuwa Mdhamini Mkuu 2026. Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la TADB na kujionea huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki.




Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi huyo, alipokuwa akizungumza























Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA