MBUNGE JIMBO LA CHALINZE AFANYA VIKAO JIMBONI KWAKE
Mbunge wa jimbo la Chalinze Akbaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amekutana na kufanya mkutano na Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakiwemo Watendaji Kata, Maafisa Tarafa, Wakuu wa Idara za Halmashauri ya Chalinze na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Ramadhani Possy.
Mbunge huyo alisema Kikao hicho kimewapa nafasi ya kujadili kwa pamoja majukumu na mipango ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo itawezesha Halmashauri ya Chalinze kutoa mchango wake mkubwa katika ustawi wa Taifa kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa.

Ridhiwani aiwahakikishia watendaji kwamba atajitahidi kulitumikia jimbo hilo kwa nguvu zake zote alizomjalia mwenyezi mungu hadi hapo atakapompumzisha aunatakapoona panafaa kupumzika.
"Tuchape kazi kwa pamoja tuwaletee maendeleo wananchi wanayotaka kuyaona, mimi nimechaguliwa na wananchi, kuwatumikia ninyi mmeajiliwa kuwatumikia tukiunganisha maalifa yetu na tukimtanguliza mungu bila shaka tutafanikiwa, mimi mtumishi mvivu sitamvumilia pia atakaye taka kukwamisha maendeleo ya wananchi jimboni", alisema Ridhiwani.
#KaziNaUtu #TunasongaMbele

.jpeg)

Comments
Post a Comment