JWTZ LAWAAGA MAJENERALI 17 JIJINI DODOMA

Magari maalumu  yaliyobeba  maafisa jenerali  17 wastaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), yakisukumwa katika hafla ya kuwaaga iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo jijini Dodoma Julai 10, 2026.
Askari wakiwa wamejipanga tayari kupita katikati magari maalumu yaliyowabeba maafisa Jrnrrali wastaafu
Jenerali Mkunda akiagana na Meja Jenerali Mstaafu Suleiman Mungiya Mzee. Aidha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda amewaasa maafisa jenerali  17 Wastaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kuacha kuhangaika na mambo ya siasa na mengineyo, bali watulie waishi vizuri na familia zao.

Pamoja na mambo mengine Jenerali Mkunda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwaaga maafisa Jenerali hao  katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo jijini Dodoma Julai 10, 2026.
Jenerali Mkunda (aliyekaa mbele katikati pamoja na viongozi wengine)  wakiwa katika picha ya kumbukumbu na  maafisa jenerali wastaafu walioagwa.
Askari wakipita kuwaaga majenersli hao

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI