WAZIRI DKT. GWAJIMA AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YAKE SHANGWE ZALINDIMA BUNGENI DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amenena kwamba ukatili wa kijinsia bado ni changamoto kubwa inayokwamisha wanawake na wanaume kufikia ndoto zao za maendeleo na ustawi wa maisha yao, licha ya juhudi mbalimbali zinazo chukuliwa na Serikali.

Akisoma bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Gwajima amesema takwimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono kwa jinsia zote yamepungua kutoka 12,749 mwaka 2024 hadi matukio 11,625 mwaka 2025. Ameeleza kuwa kupungua kwa matukio hayo kunadhihirisha mafanikio ya kampeni za uhamasishaji, elimu kwa umma na hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Hata hivyo, amesema wanawake bado ndio waathirika wakuu wa ukatili wa kingono ikilinganishwa na wanaume.

Takwimu zinaonyesha wanawake 10,976 walifanyiwa ukatili wa kingono mwaka 2024 na 10,057 mwaka 2025, huku wanaume walioathirika wakiwa 1,773 mwaka 2024 na 1,568 mwaka 2025.

Dkt. Gwajima amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, jamii na wadau wa maendeleo katika kupambana na ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha mazingira salama yanapatikana kwa wanawake, wanaume na watoto, jambo litakalowezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa. Aidha Waziri huyo amemsifu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuipa misaada ya hapa na pale wizara yake na hadi sasa imeweza kufanikiwa pakubwa hiyo yote ni jitihada zake mheshimiwa Rais, pia amewapongeza wafanyakazi wa wizara hiyo kwa kumpa ushirikiano mkubwa yeye na Naibu wake  Merypriska Mahundi, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakimu Maswi.






Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakimu Maswi akiwa  bungeni kusikiliza bajeti ya wizara yake














Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Wizara hiyo, Hawa Mchafu, akisoma ripoti ya kamati hiyo








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?