MBUNGE WA MBOGWE FAGASON AONYESHA UFAHARI WA WATOTO WAKE BUNGENI. WABUNGE WAMSHANGILIA

Mbunge wa Mbogwe mkoani Geita, Fagason Nkingwa, ameleta watoto wake leo bungeni wapata 15, amewataka vijana wasiogope kuzaa kwani Bara la Afrika ni kubwa linahitaji nguvu kazi. Mwenyekiti wa Bunge Deo Mwanyika,, akiwatambulisha watoto hao alisema alimwandikia barua kwamba watoto wake wapo 15 wamekuja kutembelea bunge kwa kujifunza, ilikuwa furaha na velegele vilitawala ukumbi wa wabunge  na badae walienda kutembelea maeneo mbalimbali ya bunge. Akizungumza na mwandishi wetu Fagason alisema anamkumbuka, marehemu Dkt. John Magufuli, aliwaomba Watanzania wazae yeye anajenga Mashule na Hospitali na kujenga Mabarabara, Fagason alitolea mfano wa baadhi ya nchi za Ulaya hivi sasa wanatoa zawadi kwa vijana wao kuzaana kwani wamebakia wazee nguvu kazi imeisha wanataka kutawaliwa na vijana kutoka mataifa mengine waliyoyatawala siku za nyuma.


















 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU