JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LAWAITA KIDATO CHA SITA KUANZA MAFUNZO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka wahitimu wa kidato cha sita Tanzania Bara na Visiwani waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria kuripoti katika makambi waliyopangiwa ili waweze kuanza mafunzo ya uzalendo,ukakamavu ,kufundishwa nidhamu,Umoja wa Kitaifa,Stadi za kazi na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa pasipo kulinyongonyesha.
Akizungumza na Wanahabari kwa niaba yake leo katika ofisi za Makai Mkuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesema majina ya waliochaguliwa yanapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz. Hii hapa ni taarifa nzima ya Mkuu huyo. TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT
KUNDI LA LAZIMA (MUJIBU WA SHERIA)
MWAKA 2026
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Nduku
Mabele, anatoa wito kwa Vijana waliohitimu elimu y a
sekondari kidato cha sita mwaka 2026, kutoka shule zote
za Tanzania Bara na Visiwani kuhudhuria Mafunzo ya JKT
Kundi la Lazima (Mujibu wa Sheria) kwa mwaka 2026.
Sanjari na wito huo, JKT limewapangia Makambi watakayo
kwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti
makambini kuanzia tarehe 0 1 Juni hadi tarehe 0 7 Juni
2026.
1
Vijana hao wamepangwa katika Kambi za JKT zifuatazo;
Rwamkoma JKT-Mara, Msange JKT-Tabora, Ruvu JKT na
Kibiti JKT-Pwani, Mpwapwa JKT na Makutupora JKT-
Dodoma, Mafinga JKT-Iringa, Mlale JKT-Ruvuma, Mgambo
JKT na Maramba JKT-Tanga, Makuyuni JKT n a Oljoro JKT-
Arusha, Bulombora JKT,Kanembwa JKT n a Mtabila JKT-
Kigoma, Itaka JKT-Songwe, Luwa JKT n a Milundikwa JKT-
Rukwa, Nachingwea JKT- Lindi na Chuo cha Uongozi JKT
(CUJKT) Kimbiji- Dar es Salaam.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho
(Physical disabilities) waripoti katika Kambi ya Ruvu iliyopo
Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya
kuwahudumia watu hao.
Aidha, JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa
vifuatavyo:
1. Bukta ya rangi ya 'Dark Blue' yenye mpira
kiunoni (lastic) iliyo na mfuko mmoja
nyuma, urefu inayoishia magotini, isiyo na
zipu.
2. T-shirt ya rangi ya kijani.
3. Raba za michezo zenye rangi y a kijani au
blue.
4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue
bahari.
2
5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa
Mikoa yenye baridi.
7. Track suit ya rangi ya kijani au blue.
8. Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili
wa kujiunga n a Elimu ya juu, zikiwemo vyeti
vya kuzaliwa, Vyeti vya kuhitimu kidato cha
nne n.k
9. Nauli ya kwenda kuripoti makambini na
kurudi nyumbani.
Orodha kamili ya majina ya vijana hao, Makambi ya JKT
waliyopangiwa, maeneo Makambi hayo yalipo na vifaa
wanavyotakiwa kwenda navyo, inapatikana katika tovuti ya
JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz
Aidha, ili kufahamu kambi kijana aliyopangiwa, atatakiwa
kuingiza jina la shule au namba ya shule aliyohitimu elimu
ya kidato cha sita, mbele ya jina la shule yake ataona neno
lililoandikwa waliochaguliwa, akichagua neno hilo ataona
majina ya waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa
Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2026, ikionesha kambi
aliyopangiwa, Wilaya na Mkoa ilipo kambi hiyo.
Ili kuona majina yote ya Vijana na kambi walizopangiwa,
mtumiaji atapakua JKT PDF 2026 iliyopo juu kulia katika
ukurasa huo.
3
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele,
anawakaribisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita
nwaka 2026 ili waweze kujiunga n a vijana wenzao katika
kujengewa Uzalendo, kufundishwa Nidhamu, Ukakamavu,
Umoja wa kitaifa, Stadi za Kazi, Stadi za Maisha na utayari
wa kulijenga na kulitumikia Taifa.
Suncol Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari n a Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Baadhi ya Makamanda wa Jeshi hilo wakifatilia hafla hiyo
Wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
Comments
Post a Comment