MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA BANGI YAONGOZA KUKAMATWA NCHINI======PROFESA KABUDI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Uremavu) Profesa Palamagamba Kabudi, akizungumza na wanahabari leo katika ukujmbi wa Bune jijini Dopdoma pale alipookuwa akizungjmzia Taarifa ya hali ya Dawa za Kulevya kwa mwaka 2025. Akiwa ameambatana na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, alisema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanaendelea kuimarika nnchini kwa mwaka 2025, hiyo ni kutokana na uwezeshwaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais huyu ameimalisha utekelezaji wa mikakati ya Kitaifa kupambana na dawa za kulevya pale alipoiwezesha tume hiyo kuendesha oporesheni zake za mara kwa mara kudhibidi ukamataji na uteketezaji wa mara kwa mara unapojitokeza. Mwaka 2025 jumla ya tani 1,074.74 za dawa za kulevya zilikamatwa katika oporesheni  zilizofanyika katika maeneo mbalimbnali nchini. Hebu soma taarifa hiyo ya waziri ujionee mwenyewe,TAARIFA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, URATIBU NA WENYE ULEMAVU) MHE. PROF. PALAMAGAMBA J.A KABUDI (MB), KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HALI YA DAWA ZA KULEVYA KWA MWAKA 2025. TAREHE: 29 MEI, 2026 MAHALI: DODOMA Ndugu waandishi wa habari, Leo nimewasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya nchini ya Mwaka 2025. Uwasilishaji wa taarifa hii ni utekelezaji wa Kifungu cha 66 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015, inayoiagiza Serikali kuandaa na kuwasilisha bungeni taarifa hiyo kila mwaka. Lengo ni kuonesha uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi kupitia Bunge, pamoja na kutoa tathmini ya utekelezaji wa mikakati ya udhibiti wa dawa hizo kwa mwaka husika. Pia, taarifa hii inatoa nafasi kwa Bunge kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu namna bora ya kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya nchini. Ndugu waandishi wa habari, Taarifa niliyoiwasilisha leo inaonesha namna Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilivyowekeza na kuweka nguvu kubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, vyombo vya ulinzi na usalama, wadau wa ndani na nje ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla, serikali imepata mafanikio makubwa katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya. 1 Ndugu waandishi wa habari, Mwaka 2025, bangi iliendelea kuwa dawa ya kulevya iliyokamatwa kwa kiwango kikubwa zaidi ambapo jumla ya tani 1,017.26, zilikamatwa. Hata hivyo, kiasi kilichokamatwa kilipungua kwa asilimia 55.97 ikilinganishwa na mwaka 2024. Hii ni kutokana na uteketezaji wa mashamba makubwa ya bangi uliofanyika mwaka 2024 na kuimarika kwa udhibiti ikiwemo utoaji elimu kwa jamii inayojihusisha na kilimo cha bangi kuhusu madhara ya kilimo cha zao hilo. Jumla ya tani 26.36 za mirungi zilikamatwa. Kiasi hiki kiliongezeka kwa asilimia 42.88 ikilinganishwa na mwaka 2024. Ongezeko hili linaashiria kuimarika kwa operesheni za ufuatiliaji na udhibiti hususan katika maeneo ya mipaka na njia zinazotumika kusafirisha dawa hizo Kwa upande wa dawa za kulevya za viwandani, Serikali ilifanikiwa kukamata methamphetamine kilogramu 907.18, heroin kilogramu 672.23, cocaine kilogramu 4.89, MDMA gramu 178 na MDA gramu 7.82. Aidha, kwa mara ya kwanza, mwaka 2025 Serikali ilikamata tani 29.52 za aina mpya ya dawa za kulevya aina ya Kratom itokanayo na mmea unaoitwa Mitrogyna speciosa. Dawa hii iliingizwa nchini kama mbolea, baada ya uchunguzi ilibainika kuwa ni dawa za kulevya. Mafanikio haya yametokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kudhibiti mitandao na njia za usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia Nchi kavu, anga na majini. 2 Aidha, Serikali iliendelea kuimarisha ukaguzi katika vituo vya forodha, vyombo vya usafiri, kampuni za usafirishaji vifurushi na kwenye kampuni zinazojihusisha na biashara ya kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya kwa lengo la kudhibiti uchepushwaji. Kupitia ukaguzi huo, jumla ya tani 31.76 na lita 183.500 za kemikali bashirifu pamoja na kilogramu 2.36 na mililita 160 za dawa tiba zenye asili ya kulevya zilikamatwa. Kwa upande wa makosa ya dawa za kulevya, mwaka 2025, jumla ya mashauri 1,124 yalifunguliwa katika Mahakama mbalimbali nchini. Pamojana mashauri yaliyokuwa yakiendelea katika Mahakama mbalimbali nchini, mashauri 1,373 yalitolewa hukumu na Jamhuri ilishinda mashauri 1,058. Kadhalika, mali zenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni 3.3 zilizohusishwa na makosa ya dawa za kulevya zilitaifishwa. Ndugu waandishi wa habari, Sambamba na hatua za udhibiti, Serikali iliendelea kutoa huduma za tiba na utengamao kwa watu wenye uraibu wa dawa za kulevya. Mwaka 2025, jumla ya watu 85,425 wenye uraibu wa dawa za kulevya walipata tiba kwenye vitengo vya afya ya akili katika hospitali za rufaa za mikoa na Kanda, kliniki za MAT na nyumba za upataji nafuu nchini. Elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya iliendelea kutolewa kwa Umma kupitia kampeni mbalimbali za uelimishaji katika jamii, taasisi za elimu na vyombo vya habari ili kuijengea jamii uelewa, maamuzi sahihi na uwezo wa kujilinda dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya. 3 Katika kuimarisha ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kubadilishana taarifa za kiintelijensia, kujenga uwezo wa kitaasisi pamoja na kuendesha operesheni za pamoja dhidi ya mitandao ya usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya. Ndugu waandishi wa habari, Matokeo chanya katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanatokana na dhamira thabiti, maono na uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani chini ya uongozi wake amewekeza kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya Nchini. Naipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama, wataalamu wa afya, wadau katika mapambano na wananchi kwa ushirikiano wao uliosaidia kuyafikia mafanikio niliyoyaeleza. Ushirikiano ni silaha muhimu katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwani mafanikio ya kweli yanahitaji juhudi jumuishi kati ya Serikali, taasisi binafsi, wadau wa kimataifa na jamii kwa ujumla. Pamoja na hayo, naomba wananchi waendelea kutoa taarifa pale wanapohisi au kushuhudia viashiria vya biashara au matumizi ya dawa za kulevya kwa vyombo husika ili kuifanya nchi yetu kuwa mahali salama na huru dhidi ya matumizi na biashara dawa za kulevya. 



Wakiwaonyesha wanahabari lipoti iliyowasilishwa bungeni leo












 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU