NAIBU WAZIRI WANU AGAWA VIFAA VYA TEHAMA JIJINI DODOMA LEO

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir (kulia), akiwa ameongozana na katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Carolyne Nombo baada ya kugawa vifaa vya TEHAMA kwa wawakilishi wa shule za msingi na za Amali nchini. ambapo alisema kuwa jitihada za Serikali za kuimarisha elimu kwa baadhi ya shule nchini imekuwa ikipokelewa vyema na. alibainisha kwambaVifaa hivyo vinatarajiwa kutumika kufundishia na kujifunzia, ili kusaidia wanafunzi kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha Wanu alitoa angalizo kwa walimu waliopokea vifaa hivyo kuhakikisha vifaa hivyo haviendi kukaa stoo bari viwe vya kujifunzia ili wanafunzi waendane na teknolojia ya sasa wasiachwe nyuma

Hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo imefanyika leo, Machi 30, 2026, katika viwanja vya ofisi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mtumba jijini Dodoma.

Vifaa hivyo vina thamani ya takribani shs milioni 769 na vitagawiwa katika shule 19 za msingi na sekondari, katika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Iringa, Ruvuma, Arusha, Geita, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara, na Kusini Unguja




Naibu Waziri Wanu akipiga picha na baadhi ya walimu waliofika kupokea vifaa hivyo









Naibu Waziri Wanu , akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo.

katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Carolyne Nombo, aakizungumza 









Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara hiyo  Sylvia Lupembe,akizungumza katika hafla hiyo
Wema na Nombo wakibadilishana mawazo




Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?