MASHIMO KATIKA BARABARA YA DODOMA SINGIDA KAZI YA TANROADS KUYAZIBA----- MHANDISI MLAVI

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi (pichani),amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuziba mashimo yaliyopo katika barabara ya kutoka Dodoma hadi Simgida, ambapo amebainisha kwamba Serikali ya Rais Samia   imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya barabara na madaraja ili kukuza uchumi wa taifa na kurahisisha usafirishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO amesema kuwa uwekezaji huo umeimarisha kwa kiasi kikubwa kuchochea biashara za ndani na za kikanda.

Aidha, amebainisha kuwa barabara ni mhimili mkuu wa uchumi kwani zaidi ya asilimia 80 ya usafirishaji wa mizigo na abiria hutegemea barabara, hali inayosukuma Serikali kuendelea kuimarisha sekta hiyo.

Pia ameongeza kuwa hadi Desemba 2025, mtandao wa barabara nchini umefikia kilomita 182,164.41, huku TANROADS ikisimamia kilomita 37,734.41 za barabara za kitaifa.

Aidha, amebainisha kuwa miradi ya barabara yenye urefu wa kilomita 5,769.74 inaendelea kutekelezwa, huku miradi mikubwa 79 yenye thamani ya zaidi ya trilioni 6 ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Pia ameongeza kuwa madaraja makubwa nane yamekamilika kujengwa ikiwemo Daraja la J.P. Magufuli na Daraja la Tanzanite, huku mengine 17 yakiendelea kujengwa nchini.


Wanahabari wakimsikiliza na kumuuliza maswali Mhandisi huyo








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?