CAG KICHERE AMKABIDHI RAIS SAMIA RIPOTI YA UKAGUZI KWA MWAKA 2024 NA 2425


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 kutoka kwa Charles Kichere, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na  Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA),  baada ya kuzipokea leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, Machi 30, 2026, amewasilisha Ripoti Kuu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa deni la Serikali bado ni himilivu na lipo ndani ya viwango salama vinavyokubalika kimataifa.

Aidha amebainisha kuwa thamani ya sasa ya deni lote la umma kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.7, ikiwa chini ya ukomo wa asilimia 55, huku deni la nje kwa Pato la Taifa likiwa ni asilimia 24.9 chini ya ukomo wa asilimia 40.

Amesema kuwa deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 125.5, ambalo bado lipo ndani ya kiwango cha asilimia 180.

Aidha amebainisha kuwa deni la Serikali limefikia Shilingi trilioni 110.05 kutoka Shilingi trilioni 97.35.

Amesema kuwa deni hilo linajumuisha deni la ndani la Shilingi trilioni 35.5 na deni la nje la Shilingi trilioni 74.55.

Aidha amebainisha kuwa mwenendo huo unaonesha kuwa ndani ya mwaka mmoja deni limeongezeka kwa Shilingi trilioni 12.73 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema kuwa ongezeko hilo limechangiwa zaidi na kuongezeka kwa mikopo ya nje pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.

Aidha amebainisha kuwa kushuka kwa thamani ya shilingi kumechangia ongezeko la deni la Shilingi trilioni 2.

Amesema kuwa ukuaji wa uchumi umeimarisha uaminifu wa Tanzania kimataifa, jambo linaloonekana kupitia ukadiriaji wa hadhi ya ukopaji ambapo nchi imepata daraja la B, huku mwezi Desemba Fitch Ratings ikitoa daraja la B+ mwezi Machi mwaka huu.san, amempongeza 

Aidha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Dkt. Charles Kichere, na watendaji wake kwa kufanya kazi nzuri iliyotukuka na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kufanya kazi bila kuchoka ili wabaini mazuri na mabaya yanayofanyika kwa watendaji wa Serikali waliopewa dhamana ya kusimamia shughuli za hapa na pale nchini.

Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali  baada ya kupokea Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Ikulu Jijini Dar es Salaam, LEO30 Machi, 202 6.

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?