WAZIRI SANGU AWAONYA WAAJIRI KUFANYA KAZI NA VYAMA VILIVYOKIDHI VIGEZO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akisalimiana na Katibu Mkuu  wa Chama cha Walimu nchinik (CWT) Mwalimu Joseph Misalaba (kushoto), baada ya kuwasili katika Kikao cha Baraza la Taifa la Chama hichi kinachofanyika jijini Dodoma na kulia ni Rais wa Chama hicho Suleiman Ikomba

Waziri Sangu amewaonya waajili akiwataka kufanya kazi na vyama vya wafanyakazi vilivyokidhi vigezo na kufuata taratibu za kuwa na wananchma ama sivyo huko mbele wasije kuanza kuilaumu serikali inawaingilia, kuna baadhi ya vyama vya walimu ambavyo vinasajiliwa kwa kuwalubuni walimu kujiunga navyo kwa kudai vitakuwa vikikata ada ya asilimi ndogo kitu ambacho kwa uendeshaji wa chama inaonekana ni uongo 


Wajumbe wa Baraza hilo wakimsikiliza kwa makini Waziri Sangu





Katibu Mkuu wa Chama hicho Mwalimu, Misalaba, akisoma hotuba ya Chama hicho , alisema kuna baadhi ya vyama vinaazishwa tena na baadhi ya waliokuwa wanachama wao  wakiwalubuni walimu kwa madai ya makato yao ni kidogo, vyama hivyo havina mchango wowote kwa Serikali hata kwa wananchi, Misalaba ameonya akisema ipo siku chama kitaanzishwa na kudai kitakuwa kikitoza ada ya mwanachama kwa Shilingi 1  kitu ambacho kwa kiuendeshaji wa chama haiwezekani, amebainisha na kusema ni kutaka kuharibu utulivu wa vyama na usalama wa nchini. "Vyama vinavyodai kuwaboleshea maslahi walimu viongozi wao wengi ni wajanja wajanja wamekalia kutwa kushinda kwenye vyombo vya habari kukipaka matope CWT, hata hivyo kwa walimu weledi hawarubuniki wanasema watakufa na CWT", amesema Mwalimu Misalaba.















Rais wa Chama hicho Suleiman Ikomba, akiishukuru Serikali kwa misaada mingi inayoipatia  CWT na kudai watazidisha ushirikiao huo  ili waliu wawe na maisha maziri hata pindi wanapotoka katika tumishi wao






Mgeni Sangu ,akipiga picha ya pamoja na staaf wa chama hicho

    





 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.