MAWASILIANO SASA KUWA KARIBU NA BURE ASEMA WAZIRI -----KAIRUKI MAWASILIANO SASA KUWA MARIBU NA BURE__________________________________________________________________________________________MAWASLIANO SASA KUWA KARIBU NA BURE _-------WAZIRI KARIUKI_______________________________________________________________________________________________________________________________
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki (Pichani) amesema kuwa Serikali imeendelea kudhibiti gharama za mawasiliano nchini ambapo gharama za kupiga simu ndani ya nchi zimeendelea kubaki shilingi 9 kwa dakika huku wastani wa bei ya data bila kifurushi ukiendelea kubaki shilingi 9.31 kwa MB moja, hali inayorahisisha wananchi wengi zaidi kumudu matumizi ya intaneti na huduma za kidigitali.
Akizungumza leo Februari 4, 2026 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100 kwa waandishi wa habari, Waziri Kairuki amesema mafanikio hayo yanatokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali katika miundombinu ya mawasiliano ikiwemo minara na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Amebainisha kuwa hali ya upatikanaji wa mawasiliano imeendelea kuimarika ambapo laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 99.3 Oktoba 2025 hadi milioni 106.9 Januari 2026 sawa na ongezeko la asilimia 7, huku watumiaji wa intaneti wakiongezeka kutoka milioni 56.3 hadi milioni 58.1 sawa na asilimia 3.
Pia ameongeza kuwa watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu wameongezeka kutoka milioni 71.7 hadi milioni 76.5 sawa na ongezeko la asilimia 6.7, hatua inayoonesha kuimarika kwa matumizi ya huduma za kifedha kidigitali nchini.
Amesema kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano ambapo wizara imekamilisha ujenzi wa minara 758 katika kata 713 nchini kwa gharama ya shilingi bilioni 166 itakayowanufaisha wananchi takribani milioni 8.5
Aidha amebainisha kuwa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wizara imekamilisha kuongeza uwezo wa minara 304 sawa na asilimia 100 ya malengo yaliyopangwa huku ujenzi wa minara 636 vijijini ukiendelea na kufikia asilimia 78 ya utekelezaji.
Pia ameongeza kuwa matumizi ya mifumo ya TEHAMA yameiwezesha wizara kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali ambapo ndani ya siku 100 imekusanya shilingi bilioni 132.2 sawa na asilimia 109.9 ya lengo, mafanikio yanayoendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidigitali na upatikanaji mpana wa huduma za mawasiliano nchini.
Comments
Post a Comment