CHUO CHA IAA ARUSHA KUFUNGUA MATAWI MIKOANI ----PROFESA SEDOYEKA

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa. Eliamani Sedoyeka, akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma. akizungumzia kuazishwa kwa masomo mbalimbali yatakayokidhi kiu ya vijana kujitegemea ambapo chuo hicho kinafungua matawi mikoani ili kuondoa kasumba ya vijana wengi kukimbilia mijini kufuata masomo. Amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukipa nyezo za kukidhi mahitaji ya chuo ambapo kinasomesha walimu wake wengi kwa kiwango cha PHD  ili wakilejea weweze kuboresha  elimu inayotolewa hapo.

 Aidha chuo hicho kimetenga Shilingi bilioni 2 kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya kiteknolojia na kidijitali, hatua inayolenga kubadili mfumo wa utoaji elimu na kuendana na mahitaji ya dunia ya sasa.

Mkuu wa Chuo huyo amesema uwekezaji huo unahusisha uanzishwaji wa Madarasa Mahiri yanayotumia Akili Unde (AI Smart Classrooms) katika kampasi za chuo hicho.

Amesema madarasa hayo yana ubao shirikishi wa kidijitali, mifumo ya kurekodi mihadhara kwa usaidizi wa AI, uchambuzi wa papo kwa papo wa ushiriki wa wanafunzi na mifumo ya kisasa ya kufuatilia mahudhurio, hali inayomwezesha mhadhiri kubinafsisha ufundishaji kwa kutumia takwimu za ujifunzaji huku wanafunzi wakipata uzoefu wa elimu shirikishi na jumuishi, ikiwemo kwa wanafunzi wa masafa.
Chuo kinaanzisha Kituo cha Kisasa cha Data kitakacholinda taarifa za kitaasisi, kusaidia majukwaa ya ujifunzaji yanayotumia ‘cloud’, kuhifadhi data za utafiti na kuimarisha usalama wa mtandao, hatua itakayopunguza utegemezi wa huduma za upangishaji wa nje na kuimarisha uhuru wa kidijitali.


Wanahabari wakimsikiliza mku huyokwa umakini mkubwa






 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.