KIHONGOSI AMTAKA MZEE WARIOBA AACHE KUSEMA SEMA HOVYO.

Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenan Kihongosi ( pichani) amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu  Jaji Joseph Sinde Warioba, kupumzika  kwa amani na kujiepucha na masuala ya kuzungumza na waandishi wa Habari mara kwa mara, aliayesam hayo jijini Dodoma leo wakati akizungumzia kuanza ziara ya nchi nzima kuangalia Ahadi za chama hicho zilizotolea wa wagombea wake kwenye kipindi cha kampeni za uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Warioba alikutana na Rais Dkt. Samia baada ya kutoka Ikulu kesho yake anazungumza na Mwanahabari kitu ambacho anafahamu taratibu zake kama alikuwa hajaridhika ageweza kupeleka dukuduku lake sehemu husika na kusikilizwa.

Aidha amempongeza Rais na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokutana na mabalozi na kuwaelezea hali halisi ya nchi hii kama msemaji wa chama anajiona Fahari kuwa na Rais kama huyo,


Amesema kuwa CCM itaendelea kusimamia misingi yake kwa kuhakikisha ukweli wa historia ya taifa na mafanikio yaliyopatikana yanabaki kulindwa, huku chama kikiimarisha uhusiano wake na wananchi kupitia kusikiliza na kutatua changamoto zao.

‎Aidha, Kihongosi , amesema kuwa chama kinatarajiwa kuanza ziara ya kimkakati nchi nzima itakayozinduliwa rasmi Januari 19, 2026 wilayani Manyoni mkoani Singida. Amesema kuwa ziara hiyo itahusisha kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Singida pamoja na kufanya mikutano ya hadhara.

Amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kuwafikia wananchi wa ngazi ya chini, kusikiliza kero zao na kuzitatua, kuisimamia Serikali, kuimarisha uimara wa chama, pamoja na kufuatilia ‎utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha amebainisha kuwa kupitia ziara hiyo, chama kitafuatilia utekelezaji wa ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizozitoa wakati wa kampeni, ikiwemo ahadi zilizopangwa kutekelezwa ndani ya siku 100, ili kubaini hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake au matarajio ya lini zitatekelezwa.





Wanahabari wakimsikiliza kwa umakini mkubwa katibu huyo





 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.