Posts

Showing posts from December, 2025

WAZIRI KAPINGA AZINDUWA BODI YA WAKURUGENZI YA STAKABADHI GHALA (WRRB)

Image
Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kampinga, akisoma Hotuba yake katika Hafla ya  Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Usimamizi wa Stakabadhi  za Ghala uliofanyika jijiji Dodoma leo asubuhi, pamoja na mambo mengi aliitaka bodi hiyo kusimamiza wakulima wapate mapato mazuri katika kuuza  mazao yao pindi yanapouzwa, amewaambia wajumbe wa bodi hiyo ataipima kwa utendaji kazi bora wake na siyo kwa jina lake, kuwe na  vitendo vingi na siyo maneno mengi. Viongozi wa dini wakiomba kabla ya uzinduzi wa bodi hiyo Meza kuu wakisisima kwa dakika moja kuombeleza kifo  cha Mbunge Jenista Mhagama Waziri Kapinga akibadilishana mawazo na  Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde Katibu Mkuu  Wizara ya Viwanda na Biashara.   Dkt. Hashil Twaib Abdallah, akaizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Kilimo Devid Silinde, akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya   Wakurugenzi   wa Bodi ya   Usimamizi   wa Stakabadhi   za   Ghala Prof . Geraldine...

JAJI MKUU TANZANIA AWATAKA MAWAKILI KUTENDA HAKI

Image
Jaji Mkuu wa Tanzania  Jaji George M. Masaju amewataka Mawakili wapya waliopokelewa na kukubaliwa kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu kwa kufuata Katiba na Sheria za Tanzania ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa “Mnapokwenda kutekeleza majukumu yenu ni muhimu mkafanye kazi kwa uadilifu mkubwa na kuzingatia miongozo mbalimbali ikiwemo Katiba, Sheria na Kanuni mbalimbali.” Amesema Jaji Mkuu. Sambamba na hilo, Jaji Mkuu wa Tanzania amewaeleza Mawakili hao kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi, kwa kusimamia misingi ya sheria , kanuni na taratibu, huku wakiwa sehemu ya kuendelea kulinda amani ya Taifa. “Niwaombe Mawakili mliokubaliwa na kupokelewa leo mkatende haki kwa wananchi, mkazingatie utawala wa sheria unafuatwa, pia ninyi ni sehemu ya kuilinda na kuitetea Amani ya Taifa hili.” Amesema Jaji Mkuu. Sherehe hizo za 73 za kuwapokea na kuwakubaki Mawakili wapya Kujitegemea zimehusisha jumla ya wahitimu 774. Jaji Masajim amewakumbusha mawakili Mahakamani...

JMAT YAOMBA KUFANYIKA MAOMBI YA AMANI KITAIFA

Image
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), imeomba yafanyike maombi ya kitaifa nchi nzima yatakayotanguliwa na mfungo wa siku tatu, maombi hayo yawe ya kina kwa watu wa Imani na madhehebu mbalimbali .  Hayo yote nikumuomba mungu msamaha na toba ya kweli na kumuomba mungu roho ya kutoa msaamaha tulipokosewaa na wenzetu. Hayo yamejili leo wakati Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh  Alhadi Mussa Salum, alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dodoma Pamoja na viongozi wa dini mbalimbali . Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba Taifa limepitia katika kipindi kigumusana kutokana na kadhia ya Tarehe 29.10.2025 wakati wa Uchaguzi  Mkuu nchini Tanzania, kadhia hiyo ilisababisha hasara ya roho za watu Pamoja na uharifu wa miundombinu na mali za Serikali na watu binafsi. Mwenyekiti huyo amesema baada ya kufuatilia Kamati yake imebaini kwamba mambo hayo yaliyotokea siku hizo yamesababisha  na kuleta chuki na Athari kubwa ya kisaikolojia katika akili na mioyo ya watu. Hivyo Tai...

KUNAVIONGOZI HAWAMWAMBII UKWELI RAIS DKT. SAMIA--------BUTIKU

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku, akisisiti jambo katika kongamano la Wazee lililoandaliwa na Taasisi hiyo lililofanyika jijini Dodoma leo, huku likizungumzia Haki na Amani ya Tanzania kuelekea 9 Desemba 2025. Kongamano hilo lililoshirikisha wazee , Butiku aliuliza kwa mshangao chanzo cha ghasia ya 29-11-2025 moja wapo lilikuwa watu kupotea , viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  kwanini walishindwa kumwambia ukweli  Rais ukweli kwanini watu wanapote, mtu anashushwa kwenye gari na kwenda kuuliwa hapo kunatatitizo, Butiku alisema Rais hawezi kufanya kila kitu anamambo mengi ya kufanya amewakaimisha watu kufanya kazi kwa niaba yake , watu wanapotea mhusika upo tu haiwezekani hata kidogo.