TFS YAWAKUTANISHA KWENYE MAFUNZO WADAU WA UKUSANYAJI TAKWIMU ZA ASALI NCHINI

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TFS, Hussein Jumanne Msuya, akizungumza na wanahabari wakati wa kipindi cha mapumziko kwenye mafunzo maalum ya wakusanya takwimu za uzalishaji wa asali nchini. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dodoma leo.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanzisha mafunzo maalumu ya ukusanyaji takwimu za uzalishaji wa asali, hatua ambayo inalenga kuongeza ufanisi na ukuaji wa sekta ya ufugaji nyuki nchini.
Akifungua mafunzo hayo jijini Dodoma leo Novemba 20,2025, Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Ndugu Daniel Pangalasi, alisema mfumo mpya wa ukusanyaji takwimu utamaliza changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za uzalishaji wa asali nchini .
“Kupitia mfumo huu tutakuwa na uhakika wa takwimu kuanzia zinapokusanywa hadi zinapohifadhiwa,” alisema kaimu mkurugenzi huyo.
Aidha Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS, Zainabu Bungwa, aliwataka wataalamu wa nyuki kuongeza uzalishaji bila kukata tamaa, akisisitiza umuhimu wa kujifunza mbinu za kisasa amabazo zitaongeza tija katika shughuli hizo.
Zaidi ya washiriki 25 kutoka TFS, wizara na taasisi za utafiti katika masuala ya nuki na asali wamehudhuria mafunzo hayo ya siku tatu yanayoendeshwa na mtaalamu mbobezi Victor Mgoo.


Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini wakisikiliza 

Mwendesha mafunzo hayo Victor Mgoo akisisitiza jambo kwa washiriki



Mtafiti wa ufugaji wa nyuki       kutoka Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Stanslaus Lukiko, akifafanua jambo kwa wanahabari
Afisa Utafiti Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Paskasi Mwiru, akifafanua jambo kwa wanahabari
Mhifadhi Mkuu  wa TFS, Frida Kundy, akisisiti jambo kwa wanahabari
 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.