RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mawaziri wa Wizara mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 18 Novemba, 2025.

‎@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

‎Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri  katika hafla iliyofanyika Novemba 18, 2025, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

‎Amesema kuwa viongozi hao wamekabidhiwa majukumu ya kuwatumikia wananchi, akibainisha kuwa utu na uwajibikaji vinapaswa kuanza kwao wenyewe kabla ya kuwafikia wananchi wanaowahudumia.

‎Amesema kuwa kazi ya kuanzia sasa ni kuendelea kuajibika kwa Taifa, huku akiwataka viongozi wazito wapunguze uzito ili kwenda sambamba na kasi ya utekelezaji kwa kuwa muda ni mchache.

‎Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imepanga kuanza kutekeleza miradi kwa kutumia fedha za ndani, kisha mashirika ya maendeleo yawakute wakiwa wameshaanza, hatua ambayo inalenga kuepusha ucheleweshaji wa miradi unaotokana na masharti ya washirika.

‎Aidha, Rais Samia amesema kuwa utekelezaji wa miradi ni jukumu la viongozi wote na sio jukumu la Rais pekee.

‎Pia, amesema kuwa miradi yote inapaswa kutoa matokeo chanya kwa wananchi na sio kubaki kama taarifa ofisini kwake.

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.