DODOMA PRES CLABU YAWAFUNDA WAANDISHI WAKE KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2025

Mgombea ubunge jimbo la Mtumba, Anthony  Mavunde, akifungua kongamano la wanahabri mkoa wa Dodoma lililohusisha mada kuu uchaguzi mkuu na taratibu zake kwa wanahabari ambapo watoa mada walijikita kuwahabarisha wanahari kuhusu nini kinatakiwa kufanya wawapo kwenye mikutano ya kampeni ili wawe salama.

Aidha  Mgombea Anthony Mavunde, amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanazingatia maadili na uhalisia katika kuripoti habari za uchaguzi ili kusaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi.

‎ Mavunde aliyasema hayo wakati  akifungua Mafunzo ya waandishi wa Habari kuhusu masuala ya Uchaguzi na Usalama kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya  Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (DPC),  Mavunde amesema kuwa tasnia ya habari ni nguzo muhimu hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi.

‎“Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika jamii. Taarifa isiyo sahihi inaweza kusababisha hata uvunjifu wa amani. Niwaombe tuendelee kuzingatia maadili, tusimame katika taaluma yetu na tufanye kazi kwa usawa bila upendeleo,” amesema.

‎Aidha, amewakumbusha waandishi wa habari kuwa jamii inawategemea kupata taarifa sahihi zinazozingatia ukweli na maadili ili wananchi waweze kufanya maamuzi ya busara katika kuwachagua viongozi wao.

‎“Wakati mwingine mtu anampenda mgombea na kuandika amepokewa na mafuriko ya watu, lakini picha zikionekana hazizidi watu hamsini. Hii haijengi heshima. Twendeni tuka ripoti mambo yote katika uhalisia wake na tuwasaidie wananchi kufanya maamuzi sahihi,” amesema mgombea  Mavunde.

 

Mgombea huyo amewapongeza viongozi wa Dodoma Pres Klabu kwa kuandaa kongamano hilo na kuwashirikisha wanahabari wote bila ubaguzi kituambacho klabu zingine huwabagua wenzao kwa vigezo vya kutokuwa hai (kutolipa ada). 

‎Aidha, Waziri Mavunde amewahimiza  waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuhamasishawananchi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 kwenda kupiga kura.






















































 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA