DODOMA PRES CLABU YAWAFUNDA WAANDISHI WAKE KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2025
Mgombea ubunge jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, akifungua kongamano la wanahabri mkoa wa Dodoma lililohusisha mada kuu uchaguzi mkuu na taratibu zake kwa wanahabari ambapo watoa mada walijikita kuwahabarisha wanahari kuhusu nini kinatakiwa kufanya wawapo kwenye mikutano ya kampeni ili wawe salama. Aidha Mgombea Anthony Mavunde, amewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanazingatia maadili na uhalisia katika kuripoti habari za uchaguzi ili kusaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi. Mavunde aliyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya waandishi wa Habari kuhusu masuala ya Uchaguzi na Usalama kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (DPC), Mavunde amesema kuwa tasnia ya habari ni nguzo muhimu hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi. “Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika jamii. Taarifa isiyo sahihi inaweza kusababisha hata uvunjifu wa amani. Niwaombe tuendelee kuzingatia maadili, tusi...