Posts

Showing posts from August, 2025

KAILIMA AONGOZA KIKAO NA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Image
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)  Kailima Ramadhani (pichani juu) leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.  

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA WANANCHI VIWANJA VYA MAO ZEDUNG BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR

Image
MATUKIO mbalimbali  ya picha katika mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi wakati akizungumza na Wananchi katika viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Jijini Zanzibar, baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar, katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara.(Picha na Ikulu)   MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali akizungumza na Wananchi katika mkutano wake uliyofanyika katika viwanja vya Mao Zedung Jijini Zanzibar, baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar  katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara leo 30-8-2025.(Picha na Ikulu)    

MGOMBEA WA CCM AWAPAGAWISHA WANACCM NA MASHABIKI WA CHAMA HICHO JIJINI DODOMA LEO

Image
  Matukio mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Chadulu Jijini Dodoma tarehe 31 Agosti, 2025.            Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Chadulu Jijini Dodoma tarehe 31 Agosti, 2025.  Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi za Chama hicho uliofanyika Chadulu Jijini Dodoma tarehe 31 Agosti, 2025. Akiwa na wagombea ubunge wa majimbo ya mkoa wa Dodoma Akiwanadi madiwa wa  Dodoma Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Chadulu Jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika ...

MGOMBEA MWENZA WA URAIS CCM DKT. NCHIMBI AOMBA KURA NYAMONGO TARIME

Image
  Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Jumapili Agosti 31 ,2025 ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mkutano mkubwa katika mji wa Nyamongo, jimbo la Tarime vijijini mkoani Mara. Balozi Dkt.Nchimbi pia aliwanadi wagombea Wabunge wa majimbo ya Mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijini,Mwita Waitara Pamoja na Madiwani Dkt.Nchimbi ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.