MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI ZA RAIS ALIPOKUWA AKIHAKIKI NA KUCHUKUA KITAMBULISHO CHAKE CHA KUPIGA KURA
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Kutokujitokeza kujiandikisha ni kukataa mwenyewe haki yako ya kikatiba na unapokataa haki ya kikatiba unapaswa kujiuliza kwanza je ni mzalendo? Ni mzalendo wa namna gani ambaye katiba imekupa fursa hii nenda kajiandikishe,piga kura,weka kiongozi unaehisi atakuja kukuhudumia,wewe, familia yako na ndugu zako. Kwanini unaikataa haki yako uliyopewa kikatiba kumbuka ukiikataa wenzio watakwenda kuweka yule wanaemtaka na unakosa fursa ya kushawishi wengine kuweka yule mnaemtaka kwahiyo unakuwa wewe wa kubabaisha tu na kulalamika." chini ya miti Amesema Rais Dkt. Samia baada ya kutimiza yeye takwa la kisheria na kuchukua kitambulisho chake katika viwanja vya ukumbi wa kijiji cha Chamwino karibu na Ikulu. je wewe mwananchi wa nchi hii huru kwanini usijitokeze kutimiza na wewe takwa hilo. kazi kwako mwaka huu kumbuka uchaghuzi upo.
Akiwahutubia wananchamwino na kuwaahidi atapiga kura hapohapo
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais
Wanasiasa wakongwe nao walikuwepo Luhavi na Burembo
Akiwaonyesha wanahabari kitambulisho chake baada ya zoezi kumalizika.
Akiwahutubia wananchamwino na kuwaahidi atapiga kura hapohapo
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais
Wanasiasa wakongwe nao walikuwepo Luhavi na Burembo
Akiwaonyesha wanahabari kitambulisho chake baada ya zoezi kumalizika.
Comments
Post a Comment