WAZIRI BASHE AWATOLEA UVUVI WAZUSHI WANAODAI CHAI YA TANZANIA KUKOSA UBORA KWENYE SOKO LA KIMATAIFA

WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amelaani madai kwamba chai ya Tanzania haiuziki Duniani, na kueleza wazi kuwa huo ni uzushi mkubwa na kusema watu hao walaaniwe.

Akizungumza leo  kwenye mkutano mkuu wa wadau wa Tasnia ya Chai, Waziri Bashe amefichua kwamba uchunguzi wake umeonyesha kuna mahitaji makubwa ya chai ya Tanzania, lakini viwanda vyetu vinakabiliwa na changamoto za ubora.

Waziri Bashe amesisitiza kuwa, umuhimu wa kuboresha mchakato wa uzalishaji ili bidhaa yetu iweze kushindana kimataifa. kulishika soko la hilo ni viwanda na wakulima kutimiza wajibu wao, wakulima walipwe haki zao na wazalishaji nao wazalishe bidhaa iliyo bora.

"Tunahitaji kushirikiana kwa dhati kabisa kama wadau ili kuimarisha tasnia hii ya chai hapa nchini," Bashe alisema



Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deo Mwanyika,akizungumza katika Kongamano hilo alidai kilio kikubwa wanachokumbana nacho pindi wanapotembelea katika maeneo ya kilimo cha Chai ni wananchi kutolipowa stahiki zao na baadhi ya viwanda vilivyoaminiwa  na Serikali wakapewa kuviendeleza ili wanunua mazao hayo kwa wakulima. Aidha amemsifu Waziri Bashe kwa kuwa mkweli asiyepindisha pindisha maneno akihimiza zao hilo lishike namba moja kimataifa na kitaifa.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Chai Tanzania, Abdulmajid Nsekela amesema anahitaji kuoana sekta ya chai inakuwa na kuchangia pato la nchi na hata kwa mtu moja mmoja, kwa uongozi wake atahakikisha lengo lenafikiwa kwa kushirikiana na bodi yake pamoja na wadau wa zao hilo kwa pamoja wataweza.

"Hii iko wazi moja ya kazi sekta binafsi ni pamoja na kuleta mabadiliko chanya na ndio maana leo hii tupo hapa lengo kuu ni kuhakikisha tunafanya au kuendesha chai kibiashara zaidi, " Amesrma







Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Rungwa, Jafari Haniu amesema Wilaya hiyo imekuwa ikIlima chai  kwa wingi lakini wakulima wa Rungwe wamekuwa na kulio cha kila siku bei ndogo ya majani mabichi ya chai. na wengine kutaka kumpelekea familiazao nyumbani kwake kwa kutokuwa na fedha za kuwahudumia

Kilio kingine cha wakulim wa Rungwe ni pamoja kucheleweshwa kwa mlipo hadi muda wa miezi sita. 

"Hivyo kupitia mkutano huu naomba utoke na majibu juu ya wakulima hawa kwani wengine wanadiriki kutaka kuniletea familia zao nizitunze kwani wao tegemeo lao ni kilimo cha zao la chai huku kilio kingine kikiwa ni mashamba kutelekezwa,"Amesema Mkuu wa wilaya huyo, na Kuitaja Kampuni ya Mohamed Enterprises (METL)  kuhusu mashamba ya chai na viwanda vilivyokabidhiwa kwao tangu mwaka 2007,kutokuwa na tija kwa wananchi wa Wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.


















 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.