HEBU TUJIKUMBUSHE KIDOGO KUHUSU FRANCO
Miaka 36 bila Franco: Mjadala wa kumuenzi nguli wa rhumba DRC waendelea

Chanzo cha picha, Getty Image
Na Mbelechi Msochi KinshasaLeo Oktoba 12, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Afrika na dunia wanamkumbuka mwanamuziki nguli na kiongozi wa bendi ya TPOK Jazz, Franco Luambo Luanzo Makiadi aliyefariki dunia miaka 35 iliyopita akiwa na umri wa miaka 51.
Nguli huyo wa muziki wa rhumba wa DRC aliyefariki mwaka 1989 nchini Ubelgiji, alikuwa alisifika mno kwa utunz wa nyimbo, uimbaji na upigaji wa ala za muziki hususan gitaa kwa
Luambo aliacha watoto kumi na nane ambao walizaliwa na wanawake tofauti.
Miongoni mwa watoto kumi na nane, Emongo Luambo ndiye mtoto pekee wa kiume ambaye pia alirithi bendi ya OK Jazz. Emongo Luambo ameiambia BBC kwamba haikuwa rahisi kumuona baba yao nyumbani, maisha yake ilikuwa ya kusafiri kila wakati.
“Baba yangu alikuwa kama wazazi wote, alikuwa amejibu haja zetu zote mimi na mandugu zangu, kibaya ni kwamba hakukuwa nasi nyumbani muda mrefu, tulikuwa tunakaa miezi nane bila kumuona ana kwa ana, watoto wengi wa wasaani wanaweza shuhudia hali hiyo, alikuwa anasafiri kila mara na akirejea nyumbani, tulikuwa tunakaa naye wiki moja tu kasha anasafiri tena lakini muda mfupi tulikuwa tunakaa naye ushirikiano ulikuwa nzuri, nafanya kila liwezekanalo kumutolea heshima katika siku kama hii” anaeleza Emongo.
Mjadala wa kukuzwa na kuenziwa kwa mziki wa Luambo
Katika pita pita zangu kwenye mitaa ya jiji la Kinshasa, nilibaini kuwa baa moja
ambapo wanapiga muziki wa zamani pekee hususani wa Luambo
Makiadi.
Wengi waliokuwa kwenye sehemu hiyo ni watu wazima waliokuwa ni wastani wa umri wa miaka sitini au zaidi.
Mmmoja wa watu hao ni Gorby Ramadhani ambaye aliniambia kwamba ana mashaka ya muziki wa Luambo kupotea kabisa kutokana na kuzuka kwa kizazi kipya, ambacho hakipigi tena muziki wa rhumba wa aina ya Luambo.
Anaeleza: Siwezi pitisha siku tatu bila kufika hapa kusikiliza muziki wa Luambo, huu wa vijana wapya sijitambui (siuelewi) kwa ndani, lakini wa Luambo, nimejitambua (nauelewa) kabisa, nilianza kuusikiliza ningali shule ya sekondari na hadi sasa sioni muziki mwingine unaoweza kulinganishwa na wa Luambo”
Bia yake kwenye meza, Ramadhani anapenda sana muziki wa testament (zamani)
“Hapo Luambo anaswali (anamuomba) Mungu, wakati tumefariki tunakwenda wapi, Mungu angetuambia kwanza siri hiyo, unaona una mke wako kisha amefariki ingekuwa vema Mungu atupe siri. Hapa Kongo hakuna wenye kumuiga, kidogo ni mwana muziki wa Kongo ya ng’ambo, Kongo Brazzaville, bwana Yulu Mabiala, hapa kwetu sioni mtu. Mtoto wake ambaye alirithi bendi sioni kitu amefanya kabisa”
Hata hivyo vijana wana mawazo tofauti na ya mzee Ramadhani kuhusu muziki wa kizazi kipya nchini DRC.
Mmmoja wa vijana hao Lykoson Risasi ambaye anapiga muziki kwa miaka kumi sasa. Anasema, uwe wa muziki wa Injili au wa muziki wa kidunia, wanamziki wengi wanaendeleza muziki wa Luambo Makiadi
“Kama leo tuko katika njia nzuri ya muziki ni kwa sababu tulifuata nija ya yule baba, siwezi kukuambia kama nafanya aina gani ya muziki lakini nakuambia hata ijapokuwa nafanya aina nyingine ya muziki, hii rhumba ambayo Luambo Makiadi alifanya inajikuta (inakuwemo) katika muziki wote, dunia mzima wanaiga mziki wake, na wanaendelea kusikiliza aina yake ya muziki, iwe wale wanaofanya muziki wa Mungu, wanaweka rhumba ndani, kusema sisi tunatupilia mbali muziki wa Luambo ni si kweli”
Mtoto anavyomuenzi baba yake
Mtoto yake Emongo Luambo ambaye ni mrithi wa bendi ya TPOK Jazz alisema, alifufua bendi ya baba yake miaka nane au tisa hivi iliyopita baada ya serkali kujenga mnara wa baba yake katika mtaa wa Matonge, sehemu iliyojulikama kama eneo la wanamuziki.
“Muziki wa Franco ulikuwa umesikika tu ndani ya gari wakati unaweka CD, wakati yeye mwenye baba yangu alikuwa anapiga live (mubashara), nikaamua kukusanya wanamuziki wafuasi wa aina yake ya muziki, nimekuambia hivi kila jumapili tunapiga muziki sehemu alipokuwa anafanya mazoezi pale panaitwa 1234, tumefanya hivi ili vijana wa kizazi kipya wajitambue katika muziki wake, tuliongeza mchuzi juu (vionjo) yaani aina aina ya muziki wa kizazi kipya”
Mwanahabari pia mtalamu katika historia ya muziki, Profesa Antoine Manda Chebwa alisema muziki wa Luambo tayari ulikwishaenea duniani kote hivyo ni vigumu kufutika au kusahaulika.
Anasema inabidi kutupilia mbali mjadala huu kuhusu mashaka ya kusaulika kwa muziki huu wa rhumba wa nguli Luambo Makiadi.
“Luambo Makiadi tupende tusipopende, anabaki kuwa mmoja wa wasanii wakubwa wa muziki wa Kongo ambaye bado yupo maarufu duniani kupitia muziki wake, yeye ni sauti sauti ya afrika, ni mtunzi wa nyimbo hasa mpiga gitaa mkubwa” anafafanua Profesa Manda Chebwa.
Francois Luambo Makiadi alizaliwa mnamo Julai 6, 1938, Jimboni Congo Central katika kijiji cha Sonabata, kilometa 80 nje ya mji mkuu Kinshasa. Alianza kufahamika alipoanza kuwa mpiga gitaa mwaka wa Bandidu Watamu na Bana Loningisa mwaka 1952 hadi mwkaa 1955. Aliunda kundi lake la T.P OK Jazz mwaka 1956. Alibandikwa jina la ‘mchawi wa gitaa” kama jina la utani kutokana na umahiri wake wa kupiga gitaa. Wakati anakutwa na umauti mwaka 1989, aliacha albam 150.
Miongoni mwa albam na vibao motomoto vilivyozikonga mno nyoyo za mashabiki wake ni pamoja na albam ya Mario ya mwaka 1985 na kuuza zaidi ya nakala 200,000.
Nguli huyo alifanya ziara na kutumbuiza katika maeneo mabalimbali duniani ikiwemo ndani ya Zaire, sasa DRC, Afrika, Ulaya na Marekani.
Kwa Afrika Mashariki Luambo Makiadi Franco anakumbukwa kwa ziara maarufu nchini Kenya ya mwaka 1985, wakati alipotumbuiza maeneo tofauti ikiwemo miji ya Eldoret na Kisumu.
Kadhalika Luambo alitumbuiza wakati wa ufunguzi wa michezo ya Afrika (All. African Games) Agosti mwaka 1987 kwenye uwanja wa Kasarani uliokuwa umefurika umati wa watu akiwa na wanamuziki wengine maarufu; Zaiko Langa Langa, Ana Mwle na Jermaine Jackson.
Alirekodi albam yake ya mwisho iitwayo Forever siku chache kabla ya kufariki dunia akishirikiana na mwimbaji maarufu Sam Mangwana. Kibao chake maarufu cha mwisho ni kile cha Toujours (kila mara) chenye maneno maarufu kweye kiitiko chake; muongo na mulozi ni watu wa kuchoma.
Anatambulika kama mmoja wa wanamuziki mahiri kabisa waliowahi kutokea DRC ya sasa na hata kote barani Afrika.
Luambo Makiadi alikuwa pia na tabia ya kukosoa viongozi serikalini katika muziki wake. Aliwahi kuingia matatani na waziri mmoja wa DRC, wakati ule ikitwa Zaire. Mama yake mzazi alialikwa na waziri huyo kusikiliza mwenyewe wimbo wa mtoto wake alioutunga mwaka wa 1982.
Kabla ya hapo alifungwa jela kwa miezi sita mwaka 1978 kutokana na kosa lilitoka na maudhui ya wimbo wake mmoja.
Hata hivyo, kwa kipindi kirefu kuanzia miaka ya 1970 Luambo Makiadi alikuwa mshirika muhimu wa Rais wa wakati huo, Maobutu Sese Seko, licha ya kwamba kabla ya Mobutu kushika madaraka, Luambo alikuwa mfuasi mkubwa wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zaire huru, Patrice Lumumba aliyeuawa Septemba 1960.
Mbali na kuwa mwanamuziki, Luambo pia aliwahi kusimamia klabu ya soka ya Vita Club ambayo ilitwaa ubingwa wa mashindano ya klabu bingwa (sasa ligi ya mabingwa) Afrika mwaka 1973.
Chanzo BBC

Chanzo cha picha, Getty Images
Comments
Post a Comment