HAKUNA MTANZANIA ATAKAYEKOSA HUDUMA ZA UGONJWA WA UKIMWI WAZIRI MKUU MAJALIWA
WAZIRI Mkuu , Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania
kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado ni tishio
na kiwango cha maambukizi mapya ni watu 60,000 kila mwaka
ambapo vijana wanaopata VVU maambukizi ni takribani asilimia 34.3 ya
maambukizi mapya.
Waziri Mkuu Majaliwa
ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akisoma
hotuba ya bajeti ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kusema kuwa Serikali itaendelea kuratibu shughuli za UKIMWI kwa kutoa
huduma endelevu na stahimilivu kwa WAVIU.
“Serikali
itaendelea kuimarisha Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI ili uweze kufanikisha
malengo ya nchi katika kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030, kuweka msukumo
katika kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto,kuhamasisha mabadiliko ya tabia katika jamii ili kupunguza
maambukizi mapya ya VVU,”amesema.
Sambamba
na hayo, Serikali inatambua mabadiliko ya sera za misaada
kutoka kwa baadhi ya wafadhili wa muda mrefu wa masuala ya UKIMWI hivyo
kufuatia mabadiliko hayo, Serikali inachukua hatua madhubuti kwa
kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha uwekezaji kwenye eneo la
utaoji huduma kwa WAVIU.
“Hatua hizo zenye lengo la kuwezesha Taifa
kujitegemea zitaendelea kuchukuliwa pia katika maeneo mengine,
niwahakikishie Watanzania wote, kuwa, Serikali itaendelea kuhakikisha
huduma zinazohusiana na masuala ya UKIMWI zinaendelea kupatikana na
hakuna Mtanzania atakayekosa huduma hizo,”amesema.
Comments
Post a Comment