DKT. NCHEMBA ATETA NA CEO WA BENKI YA ASOCIATE GENERALE JIJINI PARIS

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Kimataifa ya Societe Generale, Bw. Pierre Palmieri, iliyoshiriki
kugharamia mradi wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa mabehewa na vichwa
vya treni vya SGR, Makuu ya benki hiyo, Jijini Paris, nchini Ufaransa.
Na Benny Mwaipaja, Paris
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa mradi wa
treni ya kisasa, SGR, utainufaisha nchi ya Tanzania na nchi nyingine
zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam kiuchumi na kijamii kwa kukuza
biashara na uchumi katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Dkt.
Nchemba amesema hayo Jijini Paris nchini Ufaransa, alipokutana na
kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kimataifa ya
Societe Generale, Bw. Pierre Palmieri, iliyoshiriki kugharamia mradi
wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa mabehewa na vichwa vya treni vya SGR.
Aliishukuru
benki hiyo kwa kushiriki katika mradi huo wa kikanda ambao ni wa
kimkakati katika kukuza biashara na pia kuonesha nia ya kuendelea
kusaidia ujenzi wa SGR unaoendelea ambao kukamilika kwake kutafungua
fursa mbalimbali za kiuchumi.
Dkt.
Nchemba aliishauri benki hiyo kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza nchi
Tanzania katika sekta za viwanda, kilimo, nishati, ujenzi wa
miundombinu, elimu, afya na pia kushirikiana na sekta binafsi zikiwemo
benki za ndani.
Alirejea
wito wake kwa Jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania kwa
kuwekeza katika mradi huo wa SGR kwa kutoa huduma za uendeshaji ikiwemo
miundombinu ya mabehewa na vichwa vya treni ili kunufaika na soko kubwa
la biashara ya treni katika ukanda huo zikiwemo nchi ambazo zinategemea
Bandari ya Dar es Salaam, ambazo nchi zao hazipakani na Bahari.
Kwa
upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Asociete Generale, Bw. Pierre
Palmieri, alisema kuwa benki yake inajivunia kutoa mchango wake katika
kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana kwa ajili ya mradi huo mkubwa na wa
kimkakati kwa nchi ya Tanzania na Ukanda wote wa Afrika.
Bw.
Palmieri aliahidi kuwa benki yake itaendelea kuendelea kushirikiana na
Tanzania katika maeneo mengine katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na
kijamii ikiwemo sekta ya madini pamoja na ushauri wa kitaalamu katika
sekta ya masoko ya mitaji.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Kimataifa ya Societe Generale, Bw. Pierre Palmieri, iliyoshiriki
kugharamia mradi wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa mabehewa na vichwa
vya treni vya SGR, Makuu ya benki hiyo, Jijini Paris, nchini Ufaransa.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akioneshwa kitu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Kimataifa ya Societe Generale ya Ufaransa, Bw. Pierre Palmieri,
iliyoshiriki kugharamia mradi wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa
mabehewa na vichwa vya treni vya SGR, Makuu ya benki hiyo, Jijini Paris,
nchini Ufaransa. katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe.
Ali Jabir Mwadini.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Kimataifa ya Societe Generale ya Ufaransa, Bw. Pierre Palmieri,
iliyoshiriki kugharamia mradi wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa
mabehewa na vichwa vya treni vya SGR, Makuu ya benki hiyo, Jijini Paris,
nchini Ufaransa. katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe.
Ali Jabir Mwadini.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha, Paris, Ufaransa)
Comments
Post a Comment