CCM KUFIKISHA MIAKA 48 YATUMIKA KUTAMBULISHA WAGOMBEA WAKE URAIS MWAKA HUU JIJINI DODOMA--CPA MAKALLA
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), CPA .Amos Makalla, akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma , alisema kilele cha miaka 48 ya chama hicho tangu kuzaliwa kwake kitafanyika jijini Dodoma tarehe 5.2.2025. na mgeni rasmi anatalajiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan, Aidha Makalla, aliwaeleza wanahabri kuwa siku hiyo pia kitatumia maadhimisho hayo kuwatambulisha wagombea wa nafasi za juu wa chama hicho Tanzania bara na Zanzibar. Makalla,amewaomba wanachama wa chama hicho na wapenzi wachama hiocho kujitokeza kwa wingi, amesema huo sio mkutano ni maadhimisho wanaalikwa wote mageti ya Uwanaja wa Jamhuri yatakuwa wazi kuanzia saa 12 asubuhi.
Wanahabari wakimsikiliza Katibu huyo
Mkuu wa Habari wa Idara ya Uenezi wa Chama hicho AbuobakaryLiongo, akiwafafanulia jambo wanahabari
Wakteta jambo
"Njooni kwenye jambo letu mshuhudie Chama imara chama Tawala kipenzi cha wananchi wa nchi hii na Dunia kwa ujumla, chama Dume kilichotumika kukomboa baadhi ya nchi za Bara la Afrika njoni mkishuhudie". alisema Makalla.
Wanahabari wakimsikiliza Katibu huyo
Mkuu wa Habari wa Idara ya Uenezi wa Chama hicho AbuobakaryLiongo, akiwafafanulia jambo wanahabari
Wakteta jambo
Comments
Post a Comment