Posts

Showing posts from November, 2024

WAZIRI WA TAMISEMI ATAGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed   Mchengerwa, akiwasili katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwaajili ya  kutangazia matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini jana. Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwa ushindi  na kufuatiwa na Chadema. Wanahabari wakichukua tukio hilo  

RAIS DKT SAMIA SURUHU HASSAN AAUNGANA NA WANACHAMWINO KUPIGA KURA ZA KUCHAGUA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Image
Rais wa Dkt. Samia Suluhu hassan, leo ameungana na wananchi wa wilaya ya Chamwino kitongoji cha SOKOINE, kupiga kura za kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa. Upiga kura huo ulianza asubuhi majira ya saa mbili kamili na  Rais aliingia katika eneo hilo majira ya saa tano asubuhi na kuungana na wanchi kupanga foleni , akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura Rais alisema , Wananchi  wenye sifa wajitokeze, wasivunje amani wapige kura kwa maelewano siku ya leo itamalizika kwa salama Watanzania wote wawachague watu wenye uwezo wa kuwafanyia kazi. Mzee wa mtaa wa Sokoine akipiga kura Rais akiwa kwenye foleni ya kupiga kura Mbunge wa jimbo la Chamwino Deogratius Ndejembi, akizungumza na wapiga kura wake Rais akipewa karatasi za kupigia kura na karani wa uchaguzi kutoka TAMISEMI Rais akipiga kura