MKUU WA KITUO CHA ZIMA MOTO KAHAMA ATOA ELIMU YA MAJANGA YA MOTO KWA KINAMA HOSPITALINI KAGONGWA



NA PAUL KAYANDA, KAHAMA

Mkuu wa kituo ch Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Mkaguzi Msaidizi Hafidhi Omari, ameendesha semina maalum katika Kituo cha Afya Kagongwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa kina mama kuhusu vyanzo vya moto majumbani. Lengo kuu la semina hiyo lilikuwa ni kuwasaidia kina mama kujikinga na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kubwa na kuhatarisha maisha katika jamii.

Katika semina hiyo, Mkaguzi Msaidizi Omari alieleza kwa kina jinsi vyanzo vya moto kama vile matumizi yasiyo salama ya gesi, vifaa vya umeme visivyofanyiwa matengenezo mara kwa mara, na uendeshaji wa shughuli za jikoni bila tahadhari vinavyoweza kusababisha moto. Pia, alisisitiza umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto majumbani na jinsi ya kutumia vifaa hivyo endapo kutatokea dharura.

Kina mama walioudhuria semina hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina juu ya hatua bora za kuchukua ili kujikinga na majanga ya moto. Aidha, walipongeza jitihada za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kutoa elimu hiyo muhimu ambayo itawasaidia katika kulinda maisha yao na mali zao.

Mkaguzi Msaidizi Hafidhi Omari aliahidi kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu njia
bora za kuzuia na kukabiliana na majanga ya moto ili kupunguza athari zake katika Wilaya ya Kahama.



 

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA