Posts

Showing posts from September, 2024

MKUU WA KITUO CHA ZIMA MOTO KAHAMA ATOA ELIMU YA MAJANGA YA MOTO KWA KINAMA HOSPITALINI KAGONGWA

Image
NA PAUL KAYANDA, KAHAMA Mkuu wa kituo ch Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Mkaguzi Msaidizi Hafidhi Omari, ameendesha semina maalum katika Kituo cha Afya Kagongwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa kina mama kuhusu vyanzo vya moto majumbani. Lengo kuu la semina hiyo lilikuwa ni kuwasaidia kina mama kujikinga na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kubwa na kuhatarisha maisha katika jamii. Katika semina hiyo, Mkaguzi Msaidizi Omari alieleza kwa kina jinsi vyanzo vya moto kama vile matumizi yasiyo salama ya gesi, vifaa vya umeme visivyofanyiwa matengenezo mara kwa mara, na uendeshaji wa shughuli za jikoni bila tahadhari vinavyoweza kusababisha moto. Pia, alisisitiza umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto majumbani na jinsi ya kutumia vifaa hivyo endapo kutatokea dharura. Kina mama walioudhuria semina hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina juu ya hatua bora za kuchukua ili kujikinga na majanga ya moto. Aidha, walipongeza jitihada za Jeshi la Zi

Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais

Image
Mhandisi Manala Tabu Mbumba     Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia Waziri wa Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi Mheshimiwa Rais, YAH: OMBI LA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE KATIKA MANISPAA YA KAHAMA Kwa heshima na taadhima kubwa, naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru na kukupongeza, Mheshimiwa Rais, kwa juhudi zako thabiti na za kipekee zinazolenga kuleta maendeleo kwa Watanzania wote. Katika moyo huo wa kuthamini maendeleo, ninakuandikia ombi hili muhimu nikiwa kama mwananchi mzalendo na mdau wa maendeleo ya Manispaa ya Kahama. Ombi langu kuu ni ujenzi wa uwanja wa ndege katika manispaa yetu, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii kwa kiwango cha juu. Manispaa ya Kahama, inayokadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni 1 kufuatia Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, imekuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa uwanja wa ndege. Ukosefu huu unaleta vikwazo vya kiuchumi na kijamii, ambapo wakazi na waf