Ushuhuda wa Kusikitisha Wafichua Hatari ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo Kahama
Na Napaul Kayanda, Kahama Mhandisi Teostine Mwasha, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Uchimbaji Mdogo Tanzania, ameanza kampeni maalum ya kuelimisha jamii kuhusu athari mbaya za zebaki, kemikali inayotumika katika ukamataji wa dhahabu. Taasisi hiyo inalenga kuboresha mazingira ya kazi katika sekta ya uchimbaji mdogo kwa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanatumia zebaki kwa njia salama ili kupunguza madhara yake. Kwa sasa, Mhandisi Mwasha na timu yake wanahamasisha matumizi sahihi ya zebaki, kwa kuwa kemikali hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu, hususan kwa wale wanaoishi karibu na maeneo ya uchimbaji. Ameeleza kuwa serikali ya Tanzania imelidhia Mkataba wa Minamata unaolenga kupunguza madhara ya zebaki kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2030. Akizungumza kuhusu jitihada zao, Mhandisi Mwasha amesema kwamba wao kama taasisi wanahusika moja kwa moja katika kuielimisha jamii, hususan wachimbaji wadogo na familia zinazozunguka migodi. Amefafanua kuwa zebaki inaweza k