NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AWAKOSHA WANAMASUMBWE
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, akimkalibisha Biteko kuzungumza na wanamasumbwe
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt, Doto Biteko, akiwasilimia wanambogwe baada ya kuwasili akitokea jimboni kwake leo mchana, akizungumza huku akishangiliwa na umati wa watu waliojitokeza eneo hilo aliwaambia ombi la Mbunge wao linafanyiwa kazi siku si nyingi watapatiwa zahanati mpya kama alivyoomba mbunge wao, aidha kuhusu barabara ya lami aliwaambia ombi lao linafanyiwa kazi siku si nyingi barabara za wilaya hiyo zitapatiwa lami hiyo ni ahadi ya lazima itekelezwe. AIdha kuhusu Umeme aliwahakikishia wanamasumbwe hakuna umeme kukatika katika kwani hilo lilikuwa agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, alipompeleka katika wizara hiyo alimwagiza kwenda kutatua tatizo hilo la umeme hivi sasa mabo shwali.Amewaomba wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotalajiwa kufanyika hivi karibuni na wajiandae kumpa kura nyingi Rais Samia.
Aidha Mbunge wa jimbo hilo Maganga, alimwambia Biteko kura za Rais Samia katika jimbo hilo ni nyingi kwani amewakosha wanamasumbwe kwa kuwatatulia kero zao watakuwa watovu wa nidhamu kwa mema yote aliyowafanyika kuanzia kwenye madini wafanyabishara wadogowadogo wamepatiwa leseni tofauti na tawala zilizopita, maji, umeme na barabara. Hakika mama ameupiga mwingi na hawatamwangusha. Nae Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Nicolaus Kasendamila akizungumza hapo alisema Wanamasumbwe mbunge wao amewafanyia mambo mengi mazuri wanahaki ya kumpongeza ,amewataka wanaotaka kugombea jimbo hilo wajipange wasiwe na makando kando yeye na kamati yake hawanamuda wa kumsafisha mgombea wajitokeze waliowasafi na wasioanza kampeni mapema kwani watakwama mapema.
Mbunge Maganga, akizungumza
Wananchi wakimshangilia Biteko
Comments
Post a Comment