MWENYEKITI UWT, CHATANDA AMPA KONGORE MBUNGE SOPHIA MWAKAGENDA
Chatanda,akimuonyesha kanga kabla ya kumkabidhi
Wauza mboga mboga na matunda, wakijipatia chai kabla ya kuingia katika mkutano
Wajasiriamali wakijiburudisha na muziki kabla ya kuanza mkutano
Rais samia oyeee ndivyo wanavyosema Wajasiriamali hao
Mkurugenzi wa Kampuni ya SHIM Media Company Limited, Sophia Mwakagenda, akizungumza katika kongamano hilo ambalo aliliandaa yeye chini ya udhamini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Mkurugemzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa, akiwapungia mikono wajasiliamali baada ya kutambulishwa na Mwakagenda katika kongamano hilo
Wabunge wakisikiliza hotuba
Wabunge wakicheza muziki
Mwenyekiti Chatanda, akikabidhiwa kapu la mazagazaga mboga na matunda na wajasiliamali hao
Mwakagenda nae akikabidhiwa
Dkt. Chua na Sophia,wakibadilishana mawazo
Chatanda amezitaka Halmashauri nchini kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri hizo iwafikie walengwa hususani wafanyabiashara wanawake wadogo wadogo ili waweze kujiinua kiuchumi, ametoa agizo hilo , Jumamosi Mei 04.2024 wakati akizungumza na wanawake hao baada ya kusikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa wanawake wauza mboga na matunda jijini Dodoma, Anna Chacha, wakati hotuba yake katika kongamano hilo akidai changamoto ya wafanyabiashara hao kukosa mikopo wakiambiwa na taasisi za kifedha hawana vigezo vya kupatiwa mikopo , alibainisha kuwa mikopo mingi ikiwemo ya kausha damu ambayo imekuwa mwiba kwa wanawake wauza mboga mboga kujiendeleza kiuchumi na kuwa kikwazo kufikia malengo yao."Kulikuwa na changamoto ya mikopo ya Halmashauri kutowafikia walengwa husika, naelekeza Halmashauri zote nchini zitoe mikopo kwa wanawake wote walengwa wanapata mikopo hiyo bila kupindisha pindisha" -Chatanda "Natoa rai kwa serikali kuidhibiti au kusitisha kabisa mikopo ya kausha damu, ujinga hauishi, kwani inawaumiza wanawake wengi sana nchini" , alisema mwenyekiti huyo Aidha amempomgeza Mbunge Sophia Mwakagenda kwa kutekeleza irani ya chama cha Mapinduzi kwa kuwezesha wananchi hao wote kuhudhulia warsha hiyo.
Mwenyekiti Chatanda Amewaomba wabunge wote kuiga alichokifanya mbunge huyo ili wanawake wote nchini wanufaike na alichokifanya Mwakagenda. Maendeleo hayana chama na kausha damu haichagui chama wapewe elimu akina mamam hao ili wasiendelee kuibiwa.
Naye Mkazi wa Makole Mwajuma Ahthuman alimsifia Mbunge Sophia Mwakagenda kwa kuwa mfano wa wabunge bora wanawake anawakusanya hajali cha chama anachojuwa yeye ni kuwasaidia , alisema hakika ni mbunge wa kuigwa, amewaomba wabunge wa chamachake kuiga
Anasema Makongamano kama hayo anayasakia kwenye redio na TV wakikusanyana viongozi na kugawiana posho lakini Sophia amewafuata wauza mchicha na mbogambogo kwenye masoko karibu saba ya jiji la Dodoma ", Tangu nizaliwe sijawahi kuhudhulia kongamano kama hili lililoitishwa na chama au mbunge wa chama changu huwa nayasikia tu hakika mbunge huyu mtu wa watu.", alisema Mwajuma.
Chatanda, akimkabidhi Menyekiti Chacha Sh Milioni 1 kwa wauza mbogamboga na matunda
Chatanda oyee na CCM oyeeeeeee pia Mwakagenda adumuu, akisema mwenyekiti huyo baada ya kupokea fedha hizo
Tedson NNgwale, akitoa mada ya ujasiriamali katika kongamano hilo
Dkt. Albna Chuwa, akinunua kanga baada ya kutoka katika kongamano hilo
Comments
Post a Comment