BAJETI YA WIZARA YA NISHATI YAPITA BILA KUKAMATWA SHILINGI .

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko (kushoto), akiagana na  maofisa wa wizara yake na Taasisi zake baada ya kupiga nao picha ya pamoja  baada ya kupitishwa bajerti ya wizara hiyo na wabunge. Waziri Biteko tangu akiwasilisha bajeti ya wizara yake aliwakosha wabunge  vipaumbele vyake kwa ajili ya huduma za majimbo yao, hata wakati wa kuijadili wabunge wengi walikuwa wamepata ufafanuzi wa shida za umeme majimboni kwao kutoka kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo waliokuwa katika maonyesho ya wiki ya Nishati walioweka kambi kwa muda wa wiki nzima bungeni hapo. Ni waziri pekee hadi sasa aliyeweza kupitishiwa bajeri yake na wabunge bila misuguano ya hapa na pale na kutishia kuondoka na shilingi.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile, wakijadiliana jambo na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya baada ya kupitishwa bajeti ya Nishati
Mbunge Msukuma Kasheku, akiisifia bajeti hiyo
Mbunge zena Bushiri, akiisifia bajeti hiyo

 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo (katikati), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi  ya EWURA Profesa Mwandosya

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.