KUMBUKUMBU YA MIAKA 40 YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU MAREHEMU SOKOINE
Msemaji wa Familia ya Marehemu Edward Moringe Sokoine, Kipuyo Lembris, akizungumza na wanahabari ,kuhusu kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu kipenzi cha Watanzania 14.4.2024. hapo Luhindo Dakawa Morogoro mwaka 1984 ,akitokea bungeni Dodoma, alibainisha kwamba kutakuwa na misa nyumbani kwake Monduli Juu ya kumuombea , inatalajiwa kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kiserikali akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Edward Sokoine alizaliwa Jumatatu, Agosti mosi, 1938, katika mji wa "Monduli" mkoani "Arusha" alipata elimu ya kimsingi na ya kati katika shule ya "Monduli", kisha, mnamo 1956, akajiunga na shule ya "Omboy" ili akamilishe elimu yake ya sekondari.
Mnamo 1961, Edward Sokoine alijiunga na chama cha Taifa cha Tanganyika National Union (TANU), hiyo ilikuwa miezi michache kabla ya uhuru wa Tanganyika, aliendelea kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu huko nchini Ujerumani ambapo alisomea masomo ya usimamizi, tena alirudi nyumbani mwaka wa 1963.
Akiwa na umri wa miaka 27, aligombea ubunge na kushinda uchaguzi wa ubunge wa jimbo la "Maasai". Licha ya umri wake mdogo, alikuwa na akili timamu sana, ambayo ilimvutia kila mtu, akiwemo Rais Julius Nyerere, aliyemteua kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi, na baadaye akampandisha cheo kuwa Waziri wa Ulinzi wa Tanzania mwaka 1972.
Moringe alikuwa mwanasiasa aliyepambana na rushwa, wizi na unyonyaji. Alihudumu kwa vipindi viwili kama Waziri Mkuu wa Tanzania, kuanzia Februari 13, 1977, hadi Novemba 7,1980, na Februari 24, 1983, hadi Aprili 12, 1984.
Alijulikana kwa bidii katika kazi yake na hotuba zake za Hamasa zilizogusa nyoyo za wananchi, zaidi ya hayo daima alikuwa akitafuta suluhu za matatizo ya wananchi, na pia alikuwa mzalendo aliyependwa sana na jeshi tangu aliposhika nafasi ya mkuu wa Wizara ya Ulinzi.
Inaelezwa kuwa alijitoa sana katika jamii. Aliamua kutoa sehemu ya mshahara wake kusaidia wengine, na pia alianzisha mfuko wa Udhamini wa Rais, ambapo aliweka sehemu ya mshahara wake kusaidia akina mama kukopa.
Aprili 12, 1984 Edward Moringe Sokoine aliyekuwa mmoja wa viongozi bora nchini alifariki Dunia kwa ajali mbaya ya gari njiani Dodoma-Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 45 na kuacha Wake wawili na watoto kumi na mmoja.
Mwili wa Sokoine ulifikia Ikulu, saa kumi na moja jioni siku hiyo hiyo, ukiwa umefunikwa kwa bendera ya Kitaifa. Mazishi ya marehemu yalishuhudia heshima na taadhima, na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiongozwa na Mwalimu "Nyerere" kumuaga marehemu mpendwa, Medali zote alizopata zilizikwa pamoja naye.
Kifo cha Sokoine wakati huo kilileta mshtuko mkubwa, na sababu kuu ya hilo; kwamba alikuwa kiongozi aliyetambulika katika dhamira yake ya matumizi Bora ya Tanzania; kwa ajili ya kufikia uzalendo wa hali ya juu. Watu wengi wanasema; Sokoine alikuwa na bidii katika kazi yake, mwadilifu na muwazi, mzalendo kwa nchi yake, na alionesha uhalisia wake katika hotuba zake mbalimbali alipokuwa akizungumza na wananchi au viongozi katika matukio mbalimbali.
vyanzo:
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Comments
Post a Comment