KUMBUKUMBU YA MIAKA 40 YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU MAREHEMU SOKOINE
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa, akizungumza kabla ya kumkalibisha msemaji wa familia ya Sokoine kuzungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma leo. Msemaji wa Familia ya Marehemu Edward Moringe Sokoine, Kipuyo Lembris, akizungumza na wanahabari ,kuhusu kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu kipenzi cha Watanzania 14.4.2024. hapo Luhindo Dakawa Morogoro mwaka 1984 ,akitokea bungeni Dodoma, alibainisha kwamba kutakuwa na misa nyumbani kwake Monduli Juu ya kumuombea , inatalajiwa kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kiserikali akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Edward Sokoine alizaliwa Jumatatu, Agosti mosi, 1938, katika mji wa "Monduli" mkoani "Arusha" alipata elimu ya kimsingi na ya kati katika shule ya "Monduli", kisha, mnamo 1956, akajiunga na shule ya "Omboy" ili akamilishe elimu yake ya sekondari. Mnamo 1961, Edward Sokoine alijiunga