NHC, SEKTA BINAFSI KUJENGA MIRADI 21 YA NYUMBA YENYE THAMANI YA BILIONI 271

Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwakushirikiana na Sekta binafsi watajenga miradi ya majengo ya biashara na makazi katika eneo la Kariakoo lililopo Jijini Dar es Salaam yenye thamani ya bilioni 271.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Januari 29, 2024 na Mkurugenzina Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ahmad Abdalla wakati akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo kwa ubia na sekta binafsi iliyofanyika Upanga makao makuu ya Shirika hilo.

Amesema miradi hiyo itakuwa na tija kubwa kwenye Shirika la Nyumba kutokana na kuongeza wigo wa wafanyabiashara katika nyanja mbalimbali.

“Katika eneo la Kariakoo ambapo tunavunja nyumba 16 kwaajili ya kujenga miradi hiyo awali kulikuwa na wapangaji 190 ambapo maduka yalikuwa 118,vyumba vya makazi 72 hivyo tunategemea baadaya ujenzi kukamilika tutakuwa na wapangaji 2011, wapangaji wa maduka watakuwa 1258, vyumba vya makazi 253 na vyumba vya kuhifadhia mizigo 500”, Amesema Abdalla

Ameeleza kuwa Sera ya ubia ilizinduliwa rasm Novemba 2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao iliwawezesha kutangaza miradi takribani 87 na kati ya hiyo miradi asilimia 39 ilikuwa ni Jiji la Dar es salaam kutokana na wawekezaji Wendi kuwekeza kwenye jiji hilo.

Kwaupande wake Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Jerry Silaa, amesema utekelezaji wa sera ya ubia ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi sanajari na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 inayoelekeza kuongeza upatikanaji wa nyumba bora.

Amesema ujenzi wa miradi hiyo utahitaji kwenda sambamba na upatikanaji wa hati pacha ili kuwarahisishia Watanzania watakaonunua nyumba zilizojengwa kuwa na hati zao.

“Nazielekeza ofisi zote za aridhi za mikoa kuhakikisha wanakamilisha zoezi la utowaji wa hati kwa wakati ili watakao kuwa wamiliki wapya wa maeneo hayo wanapata hati zao”, Amesema

Mkurugenzi Mkuu wa NHC  Bw. Ahmad Abdalla akishuhudia mmoja wa wabia akisaini mikataba huo kati yake na shirika la Nyumba NHC kwa ajili ya ujenzi wa jengo katika eneo Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu Jerry Silaa akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo ya kisasa katika eneo la. Kariakoo jijini Dar  es Salaam. 

Mkurugenzi Mkuu wa NHC  Bw. Ahmad Abdalla akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kutia saini mikataba huyo kati sekta binafsi na shirika la Nyumba NHC kwa ajili ya ujenzi wa jengo katika eneo Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA