CHUO CHA TEHAMA KUJENGWA DODOMA CHENYE UWEZO WA KUCHUKUA ZAIDI YA WANAFUNZI 15000
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla akiagana na Washauri Elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang Consoltium cha Korea Kusini baada kumalizika kwa kikao cha ufunguzi wa kuanza ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Nala Dodoma, pamoja na kutangaza nafasi za ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA kwa watumishi Umma Januari 29,2024..Katibu Mkuu,Mohammed Khamis Abdulla akiwa katika picha ya pamoja na washauri elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang Consoltium cha Korea Kusini pamoja na maafisa wengine wa serikali.
Baadhi ya wakuu wa vyuo vikuu vya Tanzania wakijitambulisha.
Baadhi ya maafisa wa serikali wakiwa katika mkutano huo
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Izabela Katondo akiongoza mkutano wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Mohammed Khamis Abdulla na wanahabari katika Mji wa Kiserikali Mtumba Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mohammed Khamis Abdulla akijibu maswali ya waandishi wa habari
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Serikali imeenza mchakato wa ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 15000 katika eneo la Nala jijini Dodoma
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mohammed Khamis Abdulla baada ya kumalizika kwa kikao cha Washauri Elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang Consoltium cha Korea Kusini watakao husika na mchakato wa ujenzi huo.
Aidha, Katibu Mkuu, Abdulla ameeleza kuwa usajili wa wanafunzi watakaojiunga na chuo hicho hautakuwa na masharti magumu, kila mtanzania atakuwa huru kujiunga ili mradi awe na mwanga kidogo wa mambo ya tehama.
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu, Abdulla alitangaza nafasi 440 za ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA kwa watumishi wa umma.
Hebu fuatana na mimi hapo chini kufahamu kiundani kwa kusoma hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU MKUU ABDULLA KUHUSU MRADI HUO PAMOJA NA UTANGAZAJI WA WATUMISHI WA SERIKALI KUOMBA UFADHILI WA MASOMO YA MUDA MREFU NA MUDA MFUPI YANAYOTOLEWA NA SERIKALI KUPITIA WHMTH KATIKA MRADI WA DTP.
Ndugu Waandishi wa Habari
Karibuni katika kikao hiki cha ufunguzi wa kuanza ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Dodoma, pamoja na kutangaza nafasi za ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA kwa watumishi Umma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 12 Septemba, 2021 aliunda Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kwa mujibu wa mgawanyo wa majukumu (Instrument) kupitia tangazo la Serikali Na. 782 la tarehe 22 Novemba, 2021 pamoja na majukumu mengine Wizara imepewa jukumu la kufanya tafiti, maendeleo na ubunifu kwenye TEHAMA pamoja na kuendeleza wataalam wa TEHAMA nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inatekeleza miradi miwili ya ujenzi wa Vyuo vya TEHAMA katika Jiji la Dodoma eneo la Nala pamoja na Mkoa wa Kigoma eneo la Buhigwe. Utekelezaji wa Miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/2026 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambayo inasisitiza uwepo wa mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika TEHAMA nchini.
Mipango na Mikakati yote hii inasisitiza kuongeza ujuzi wa kitaaluma katika eneo la TEHAMA hususan mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika eneo la Teknolojia zinazoibukia (emerging Technologies). Ujenzi wa vyuo hivi vya TEHAMA vitachochea maendeleo katika wakati huu wa Mapinduzi ya 4, 5 na 6 ya viwanda ambayo ndio chachu ya ukuaji wa Uchumi wa Kidigitali Duniani.
Vyuo hivi vya TEHAMA vitakua kitovu cha taaluma, Ujuzi, ubunifu, Tafiti, Maarifa na kukuza ujasiri amali wa kidijitali Kitaifa na Kimataifa. Vyuo hivi pia vitaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri pa-kuvutia Utalii wa Kidijitali, Kujifunzia, na kuongeza uwekezaji kutokana na upatikanaji endelevu wa
jamii yenye Maarifa yanayoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia Duniani.
Kwa ufupi ninaomba niwajulishe kuhusu mradi wa chuo cha TEHAMA -
Kigoma , kwamba ni moja ya utekelezaji wa miradi mingine mitatu (3) ya kijamii( Corporate Social Responsibility – CSR) ikiwa ni jukumu la kijamii la Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ambao unasimamiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Mpaka sasa eneo la Ujenzi limepatikana katika Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Michoro imekamilika na kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 80 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kinachosubiriwa ni Mkandarasi kuanza ujenzi huo.
Tarehe 14 Oktoba, 2021 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kwenye Viwanja vya Magufuli, Wilayani Chato, Mkoani Geita aliahidi kuwa Serikali itajenga chuo kikubwa cha TEHAMA ambacho kitasaidia kutoa ujuzi kwa vijana wote wanaojishughulisha na TEHAMA.
Katika kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilianza maandalizi ya ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA ambacho kinajengwa katika eneo la NALA Jijini Dodoma ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana na wabunifu nchini kuhusu masuala ya TEHAMA, kama vile Teknolojia zinazoibukia (Emerging Technologies), Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano pamoja na utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA.
Chuo hiki kitakuwa ni tofauti na vyuo vingine kwa kuwa ni chuo ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi kwa muda mfupi kwa njia ya moduli kulingana na mahitaji kwa nyakati husika na baada ya moduli kuisha muhitimu atakuwa amepewa ujuzi kwenye eneo mahususi na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija, na hii itapelekea vijana wengi kujiajiri kwa haraka au kuajiriwa katika Sekta ya Tehama kulingana na mahitaji.
Hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwani sio vijana wote wamefanikiwa kusoma darasani na kufikia kiwango cha juu, kuna vijana wenye vipaji ambao hawajasoma hivyo kupitia chuo hiki vijana wengi watapatiwa ujuzi na kuweza kuendana na mapinduzi ya 4,5 na 6 ya Viwanda.
Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo mahiri eneo la Nala Jijini Dodoma, katika hatua za awali, unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha upembuzi yakinifu pamoja na uandaaji wa mitaala na miongozo ya chuo hicho. Kwa upande wa ujenzi wa chuo hicho fedha zitakazo tumika ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Exim benki ya Korea. (Watu wa Exim Bank Korea tunao hapa)
Hadi leo tunakutana hapa masuala yafuatayo yametekelezwa;
1) Eneo la Ekari 400 kwa ajili ya ujenzi wa chuo mahiri cha Tehama limepatika katika eneo la Nala, Jijini Dodoma;
2) Mahitaji ya awali ya Chuo hicho, yakijumuisha aina ya majengo na masomo yatakayo fundishwa yameandaliwa na kuwasilishwa Korea
Exim Bank;
3) Mshauri Elekezi Hanyang University Consortium (Hayang
University Erica na Yuil Engeineering and Moon Engineering)
wamepatikana kwa ajili ya kuanza hatua za awali za ujenzi kwa
kufanya upembuzi yakinifu ambapo mshauri elekezi huyo
ameshawasili Jijini Dodoma na Timu hiyo ya Washauri Elekezi
inaongozwa na Prof. Taejoon Park ambaye amejumuika nasi leo na
mme msikia na tayari kikao cha awali “kick- off Meeting “ kimefanyika na kazi hiyo itakamilishwa ndani ya miezi sita kutoka sasa.
Leo hii tunauhabarisha umma wa Watanzania kuwa maandalizi
ya Ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama eneo la Nala Dodoma
yameanza rasmi leo tarehe 29 Januari, 2024.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa Umma mia tano (500) kwenye kozi za kuongeza ujuzi kwenye masuala yanayohusu Tehama hususani Teknolojia zinazoibukia.
Katika awamu ya kwanza jumla ya watumishi wa umma ishirini (20)
wameweza kufadhiliwa katika mafunzo ya muda mrefu katika vyuo vikuu nje ya nchi ambapo kozi walizoenda kuongeza ujuzi ni kwenye masuala yanayohusu TEHAMA hususan Teknolojia zinazoibukia.
Pia tupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kupeleka wataalamu 40 kwenye mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi ambapo kati ya hao 15 ni Maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam (5), Chuo Kikuu cha Dodoma (5) pamoja na Mbeya University of Science and Technology (MUST - 5) lengo ni kuwajengea uwezo Maprofesa hao kwenye Teknolojia zinazoibukia na watakapomaliza waweze kuendelea kutoa mafunzo katika vyuo walivyotoka na wakati Chuo Mahiri cha Tehama kinaendelea kujengwa.
Pia nafasi 15 tutazitoa kwa watumishi wa Umma kutoka kwenye Taasisi ya benki ya Tanzania (BOT (5) – block chain), Mamlaka ya Mapato (TRA (5) – Akili bandia kwenye ukusanyaji wa kodi), Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA
(5) – big data analytics pamoja na Akili bandia).
Nafasi 10 tutazito kwa Watumishi wa Umma kwenda kusoma kwenye
masoma ya Anga za Juu (Space Technology).
Leo hii nawatangazia Watumishi wa Umma uwepo wa nafasi mia nne
hamsini (440) za ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwenye masuala ya TEHAMA na Teknolojia zinazoibukia kwa Watumishi wa Umma.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - UTUMISHI (OR-MUUUB) tutaendelea kuhakikisha tunasimamia mafunzo kwa kada hii ya TEHAMA kwa watumishi wa Umma.
Hivyo basi napenda kuwatangazia watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa tumefungua dirisha la maombi hayo kupitia tovuti ya www.scholarship.go.tz.
Baada ya kutoa taarifa hiyo, nawashukuru na niwatakie majukumu mema katika kuhabarisha Umma kuhusu maandalizi ya ujenzi wa chuo mahiri cha TEHAMA kitakacho jengwa Jijini Dodoma pamoja na Ufadhili wa Watumishi wa Umma kwenye masuala ya Tehama.
Asanteni kwa kunisikiliza………
Ndugu Waandishi wa Habari Karibuni katika kikao hiki cha ufunguzi wa kuanza ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Dodoma, pamoja na kutangaza nafasi za ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA kwa watumishi Umma. Ndugu Waandishi wa Habari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 12 Septemba, 2021 aliunda Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kwa mujibu wa mgawanyo wa majukumu (Instrument) kupitia tangazo la Serikali Na. 782 la tarehe 22 Novemba, 2021 pamoja na majukumu mengine Wizara imepewa jukumu la kufanya tafiti, maendeleo na ubunifu kwenye TEHAMA pamoja na kuendeleza wataalam wa TEHAMA nchini. Ndugu Waandishi wa Habari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inatekeleza miradi miwili ya ujenzi wa Vyuo vya TEHAMA katika Jiji la Dodoma eneo la Nala pamoja na Mkoa wa Kigoma eneo la Buhigwe. Utekelezaji wa Miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa tatu wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2021/2026 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025 ambayo inasisitiza uwepo wa mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika TEHAMA nchini. 3 | Page Ndugu Waandishi wa Habari Mipango na Mikakati yote hii inasisitiza kuongeza ujuzi wa kitaaluma katika eneo la TEHAMA hususan mafunzo ya Ujuzi na Ubunifu katika eneo la Teknolojia zinazoibukia (emerging Technologies). Ujenzi wa vyuo hivi vya TEHAMA vitachochea maendeleo katika wakati huu wa Mapinduzi ya 4, 5 na 6 ya viwanda ambayo ndio chachu ya ukuaji wa Uchumi wa Kidigitali Duniani. Ndugu Waandishi wa Habari Vyuo hivi vya TEHAMA vitakua kitovu cha taaluma, Ujuzi, ubunifu, Tafiti, Maarifa na kukuza ujasiri amali wa kidijitali Kitaifa na Kimataifa. Vyuo hivi pia vitaifanya Tanzania kuwa mahali pazuri pa-kuvutia Utalii wa Kidijitali, Kujifunzia, na kuongeza uwekezaji kutokana na upatikanaji endelevu wa jamii yenye Maarifa yanayoendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia Duniani. Ndugu Waandishi wa Habari Kwa ufupi ninaomba niwajulishe kuhusu mradi wa chuo cha TEHAMA - Kigoma , kwamba ni moja ya utekelezaji wa miradi mingine mitatu (3) ya kijamii( Corporate Social Responsibility – CSR) ikiwa ni jukumu la kijamii la Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ambao unasimamiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Mpaka sasa eneo la Ujenzi limepatikana katika Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Michoro imekamilika na kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 80 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kinachosubiriwa ni Mkandarasi kuanza ujenzi huo. 4 | Page Ndugu waandishi wa Habari Tarehe 14 Oktoba, 2021 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kwenye Viwanja vya Magufuli, Wilayani Chato, Mkoani Geita aliahidi kuwa Serikali itajenga chuo kikubwa cha TEHAMA ambacho kitasaidia kutoa ujuzi kwa vijana wote wanaojishughulisha na TEHAMA. Ndugu waandishi wa Habari Katika kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilianza maandalizi ya ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA ambacho kinajengwa katika eneo la NALA Jijini Dodoma ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana na wabunifu nchini kuhusu masuala ya TEHAMA, kama vile Teknolojia zinazoibukia (Emerging Technologies), Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano pamoja na utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA. Ndugu waandishi wa Habari Chuo hiki kitakuwa ni tofauti na vyuo vingine kwa kuwa ni chuo ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi kwa muda mfupi kwa njia ya moduli kulingana na mahitaji kwa nyakati husika na baada ya moduli kuisha muhitimu atakuwa amepewa ujuzi kwenye eneo mahususi na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija, na hii itapelekea vijana wengi 5 | Page kujiajiri kwa haraka au kuajiriwa katika Sekta ya Tehama kulingana na mahitaji. Ndugu waandishi wa Habari Hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwani sio vijana wote wamefanikiwa kusoma darasani na kufikia kiwango cha juu, kuna vijana wenye vipaji ambao hawajasoma hivyo kupitia chuo hiki vijana wengi watapatiwa ujuzi na kuweza kuendana na mapinduzi ya 4,5 na 6 ya Viwanda. Ndugu waandishi wa Habari Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo mahiri eneo la Nala Jijini Dodoma, katika hatua za awali, unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha upembuzi yakinifu pamoja na uandaaji wa mitaala na miongozo ya chuo hicho. Kwa upande wa ujenzi wa chuo hicho fedha zitakazo tumika ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Exim benki ya Korea. (Watu wa Exim Bank Korea tunao hapa) Ndugu waandishi wa Habari Hadi leo tunakutana hapa masuala yafuatayo yametekelezwa; 1) Eneo la Ekari 400 kwa ajili ya ujenzi wa chuo mahiri cha Tehama limepatika katika eneo la Nala, Jijini Dodoma; 6 | Page 2) Mahitaji ya awali ya Chuo hicho, yakijumuisha aina ya majengo na masomo yatakayo fundishwa yameandaliwa na kuwasilishwa Korea Exim Bank; 3) Mshauri Elekezi Hanyang University Consortium (Hayang University Erica na Yuil Engeineering and Moon Engineering) wamepatikana kwa ajili ya kuanza hatua za awali za ujenzi kwa kufanya upembuzi yakinifu ambapo mshauri elekezi huyo ameshawasili Jijini Dodoma na Timu hiyo ya Washauri Elekezi inaongozwa na Prof. Taejoon Park ambaye amejumuika nasi leo na mme msikia na tayari kikao cha awali “kick- off Meeting “ kimefanyika na kazi hiyo itakamilishwa ndani ya miezi sita kutoka sasa. Ndugu waandishi wa Habari Leo hii tunauhabarisha umma wa Watanzania kuwa maandalizi ya Ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama eneo la Nala Dodoma yameanza rasmi leo tarehe 29 Januari, 2024. Ndugu waandishi wa Habari Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka mpango wa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa Umma mia tano (500) kwenye kozi za kuongeza ujuzi kwenye masuala yanayohusu Tehama hususani Teknolojia zinazoibukia. 7 | Page Ndugu waandishi wa Habari Katika awamu ya kwanza jumla ya watumishi wa umma ishirini (20) wameweza kufadhiliwa katika mafunzo ya muda mrefu katika vyuo vikuu nje ya nchi ambapo kozi walizoenda kuongeza ujuzi ni kwenye masuala yanayohusu TEHAMA hususan Teknolojia zinazoibukia. Pia tupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kupeleka wataalamu 40 kwenye mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi ambapo kati ya hao 15 ni Maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam (5), Chuo Kikuu cha Dodoma (5) pamoja na Mbeya University of Science and Technology (MUST - 5) lengo ni kuwajengea uwezo Maprofesa hao kwenye Teknolojia zinazoibukia na watakapomaliza waweze kuendelea kutoa mafunzo katika vyuo walivyotoka na wakati Chuo Mahiri cha Tehama kinaendelea kujengwa. Pia nafasi 15 tutazitoa kwa watumishi wa Umma kutoka kwenye Taasisi ya benki ya Tanzania (BOT (5) – block chain), Mamlaka ya Mapato (TRA (5) – Akili bandia kwenye ukusanyaji wa kodi), Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA (5) – big data analytics pamoja na Akili bandia). Nafasi 10 tutazito kwa Watumishi wa Umma kwenda kusoma kwenye masoma ya Anga za Juu (Space Technology). 8 | Page Ndugu waandishi wa Habari Leo hii nawatangazia Watumishi wa Umma uwepo wa nafasi mia nne hamsini (440) za ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwenye masuala ya TEHAMA na Teknolojia zinazoibukia kwa Watumishi wa Umma. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - UTUMISHI (OR-MUUUB) tutaendelea kuhakikisha tunasimamia mafunzo kwa kada hii ya TEHAMA kwa watumishi wa Umma. Hivyo basi napenda kuwatangazia watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa tumefungua dirisha la maombi hayo kupitia tovuti ya www.scholarship.go.tz. Ndugu waandishi wa Habari Baada ya kutoa taarifa hiyo, nawashukuru na niwatakie majukumu mema katika kuhabarisha Umma kuhusu maandalizi ya ujenzi wa chuo mahiri cha TEHAMA kitakacho jengwa Jijini Dodoma pamoja na Ufadhili wa Watumishi wa Umma kwenye masuala ya Tehama. Asanteni kwa kunisikiliza………
Comments
Post a Comment