UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.
Leo ni Miaka Mitano ya Kumbukumbu ya Kifo cha Amina Chifupa Mpakanjia Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya. Amina leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena katika Redio ya Clouds FM. Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania wataendelea kumuenzi na atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa dawa ya kulevya. Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini. ...
Comments
Post a Comment