WAOKOTA VYUMA CHAKAVU HATARINI KUPATWA NA MIONZI
Baalozi Naimi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili hapo
Mkurugenzi Busagala, akimuonyesha Maabara za Tume hiyo
Mkurugenzi akimweleza jambo kwa msisitizo Balozi
Wafanyakazi na wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Mkuu wa Idara ya Habari wa Tume hiyo akiwakalibisha wanahabari na balozi katika mkutano huo
Mkuu wa Tume hiyo Kanda ya Kati, Machibya Matulanga,akitoa maelezo kuhusu kazi za Tume hiyo
Picha zikionyesha miili ya binadamu iliyopata madhara kutokana na kukusanya vyuma chakavu
Balozi na Mkjurgenzi wakisikiliza kwa makini maelezo ya tume hiyo
Mkurugenzi wa Nguvu za Atomu nchini Profesa Lazaro Busagala, amesema wakusanya vyuma chakavu wapo katika hatari kubwa ya kupata maradhi ya mionzi kama hawatakuwa makini wakati wakifanya kazi hiyo, Mkurugenzi huyo aliyasema hayo leo wakati akimkalibisha Balozi wa Tanzania nchini Austria, Naimi Aziz (kushoto) alipotembelea Makao Maku ya tume hiyo zilizopo eneo la Kikombo jijini Dodoma. Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba wakusanya vyuma chakavu hawanabudi kuwa makini pindi wanapokusanya vyuma hivyo ama sivyo watakuwa katika matatizo makubwa ya kupatwa na maradhi mbalimbali, Pia alisema hivyo hivyo kwa wale wanaochimba visima vya maji kwa matumizi ya binadamu bila kuwashirikisha wafanyakazi wa tume hiyo ambapo maji yanayopatikana katika visima hivyo ni lazima yapimwme na watalamu wa tume hiyo ili wathibitishe kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu, Baadhi ya maji yamekuwa yakibainika kuwa na mionzi ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu kama wataruhusiwa kuyatumia.
Mkurugenzi Busagala, akimpatia zawadi Balozi Naimi baada ya kumalizika mazungumzo
Balozi Naimi,akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume hiyo baada ya kumalizika kwa kikao chao
Balozi Naimi, akizungumza na Mkurugenzi Busagala wakati akijiandaa kuondoka katika ofisi za Tume hiyo
Comments
Post a Comment